EPL: Vijana Watano Ambao Wameipokea Ligi Kuu Ya Uingereza Kwa Mikono Miwili

8th October 2019

LONDON, Uingereza -Ligi kuu ya Uingereza rasmi sasa imekamilisha mzunguko wa nane na sasa timu zitapumzika kwa muda huku wachezaji wakijiunga na timu zao za taifa kwa ajili ya majukumu mengine.

Daniel James
Daniel James
SUMMARY

Si ajabu baadhi ya timu zilianza kumuulizia kwenye dirisha la usajili lakini zikamkosa lakini moto alioanza nao msimu huu nadhani Leicester City wajiandae kupokea pesa ndefu mwishoni mwa msimu.

Ni mapema sana kuanza kutoa maksi kwa waliofanya vizuri lakini kwa hadi hapa tulipofika ni vyema kama dawati la SportPesa News kuwapa dole gumba vijana hao waliounza mwendo wa EPL kwa kishindo.

Tammy Abraham (Chelsea)

Utazungumza nini kibaya kuhusu kijana huyo raia wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria. Hivi tunavyozungumza tayari ana mabao nane kwenye ligi kuu ya Uingereza sawa na Sergio Aguero kileleni.

Unapozungumzia sifa zake pia huwezi kusahau bao lake moja alilofunga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Lille na hilo kufanya idadi ya mabao yake msimu huu kufikia 9 kwenye michuano yote.

Akiwa na umri wa miaka 19 tu tayari watu wameanza kuona kuwa huenda akawa mrithi sahihi wa mshambuliaji nguli wa zamani wa timu hiyo Didier Drogba. Ni dhahiri kabisa dili lake la mkopo ndani ya Aston Villa msimu uliopita limesaidia kukuza mpira wake.

Bukayo Saka (Arsenal)

Tangu alipofanya vizrui kwenye mchezo wa kwanza wa Europa dhidi ya Franfurt, Bukayo Saka ameteka hisia za kocha wake Unai Emery na kumuanzisha kwenye michezo yote iliyofuata.

Saka amekuwa kwenye kiwango kizuri hadi sasa akiwa amefunga bao moja na ametengeneza assist moja kwenye mchezo dhidi ya Manchester United ambapo Piere Aubamiyang alifunga bao la kuchomoa.

Mason Mount (Chelsea)

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Mason Mount, 20, amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipohakikishiwa na namba na kocha Frank Lampard.

Amerejea Chelsea kutoka Derby Country ambapo alikuwa akicheza kwa mkopo chini ya Frank Lampard na hadi sasa tayari ameshafunga mabao manne.

Daniel James (Manchester United)

Winga mpya wa Manchester United aliyesajiliwa akitokea timu ya daraja la kwanza ya Swansea City kwa dau la paundi milioni 15.

Biashara yake kuja United haikuwa maarufu sana hasa ukizingatia watu wengi walikuwa hawamjui. Hata hivyo ndani ya mechi chache tu Daniel James ameonesha kuwa yeye ni mchezaji wa aina gani.

Amefunga mabao matatu hadi hivi sasa kati ya mabao tisa yaliyofungwa na Man United msimu huu.

James Maddison (Leicester City)

James Maddison ni tofauti kidogo na wachezaji wengine hapo juu kwakuwa yeye yupo kwenye ligi kuu tangu msimu uliopita.

Alisajiliwa na Leicester City kutoka klabu ya Norwich City wakati huo wakiwa ligi daraja la kwanza. Hata hivyo kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 ameyazoeza mapema sana maisha ya EPL kiasi kwamba kuwa mchezaji muhimu ndani ya Leicester.

Si ajabu baadhi ya timu zilianza kumuulizia kwenye dirisha la usajili lakini zikamkosa lakini moto alioanza nao msimu huu nadhani Leicester City wajiandae kupokea pesa ndefu mwishoni mwa msimu.

Hadi sasa amefunga mabao mawili na yote ameyafnga kwenye mechi kubwa, moja ni la ushindi dhidi ya Tottenham na bao lake la pili amewafunga Liverpool ingawa timu  yake ilipoteza mchezo huo.

Imeandaliwa na Jerry Mlosa