EPL: Traore Apiga Mbili Wolves Wakiisasambua Man City Etihad Huku Chelsea, Arsenal Wakizoa Pointi Tatu

6th October 2019

MANCHESTER, Uingereza -Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City wameambulia kipigo cha kushtukiza cha mabao 2-0 kutoka kwa Wolves kwenye dimba lao la nyumbani la Etihad.

Adama Traore
Adama Traore
SUMMARY

Kipigo hicho cha City kinakuwa ni habari njema kwa wapinzani wao wa karibu Liverpool ambao sasa wanakaa kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya City baada ya kuitwanga Leicester 2-1 hapo jana.

Mabao ya Wolves yamefungwa na mchezaji anayetajwa kuwa na kasi zaidi nchini Uingereza, Adam Traore dakika ya 80 na dakika ya 95 ya mchezo akimegewa pande na mshambuliaji Raul Jimenez kwenye mabao yote mawili.

Kipigo hicho cha City kinakuwa ni habari njema kwa wapinzani wao wa karibu Liverpool ambao sasa wanakaa kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya City baada ya kuitwanga Leicester 2-1 hapo jana.

Nazo klabu za Chelsea na Arsenal zimeibuka na ushindi muhimu kwenye mechi za ligi kuu ya Uingereza mzunguko wa nane zilizofanyika leo.

Arsenal wao wakiwa nyumbani wamewafunga Bournermouth kwa bao 1-0 mfungaji akiwa ni David Luiz aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Nicholas Pepe.

Nao majirani zao klabu ya Chelsea wamewafumua Southampton ugenini kwa jumla ya mabao 4-1.

Kwenye mchezo huo kinda Tammy Abraham ameendeleza moto wake katika upachikaji wa mabao akifunga bao lake la nane la msimu na kumkuta kinara Kun Aguero.

Mabao mengine yamefungwa na Mason Mount, Ngolo Kante na Mitchy Batshuayi aliyeingia kipindi cha pili.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya