EPL: Tammy Abraham, Pulisic Wazama Kambani, Chelsea Wakishinda Mechi Ya Sita Mfululizo

9th November 2019

LONDON, Uingereza-Klabu ya Chelsea imeendeleza rekodi yake ya ushindi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuinyuka Crystal Palace kwa mabao 2-0

Tammy Abraham
Tammy Abraham
SUMMARY

Chelsea sasa wanakalia nafasi ya pili wakiwa na alama 26 baada ya kushuka dimbani mara 12 huku wakiiombea Manchester City mabaya kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Liverpool ili waendelee kusalia kwenye nafasi hiyo sambamba na kuiombea Leicester City mabaya usiku huu.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge, mabao ya Chelsea yamefungwa na mshambuliaji Tammy Abraham akimalizia vyema pasi ya Willian huku Mmarekani Christian Pulisic akishindilia msumari wa mwisho na kuwashuhudia vijana hao wa kocha Frank Lampard wakishinda mechi ya sita mfululizo.

Kwa matokeo hayo sasa, Frank Lampard ambaye ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba, anakuwa kocha wa sita raia wa Uingereza kushinda mechi sita mfululizo kwenye Ligi hiyo pendwa ulimwenguni.

Tammy Abraham amefunga bao lake la kumi msimu huu kwenye Ligi Kuu akimfikia Jamie Vardy ambaye timu yake ya Leicester City inakipiga dhidi ya Arsenal usiku huu kwenye dimba la King Power.