China Open: Yote Unayohitaji Kujua Kabla Ya Fainali Ya Naomi Osaka v Ash Barty Leo

6th October 2019

BEIJING, China- Leo kwenye fainali ya michuano ya tenesi ya China Open kwa upande wakina dada Naomi Osaka atavaana uso kwa uso dhidi ya Ashleigh Barty.

Ashleigh Barty.
Ashleigh Barty.
SUMMARY

Mchezo wa leo utakuwa ni wanne kwa wanadada hawa kukutana. Kwenye michezo mitatu iliyopita Barty ameshinda mara mbili na Osaka ameshinda mara moja. 

Muaustralia, Barty ndiye mchezaji namba moja kwa ubora kwa upande wa wanawake kwa sasa wakati Osaka anashika nafasi ya nne.

Mjapan, Osaka amefika fainali ya michuano hii baada ya kumuondosha bingwa mtetezi Caroline Wozniacki pia kwenye robo fainali akimuondosha bingwa wa US Open, Bianca Andreescu wakati Barty ambaye ni bingwa wa France Open amemfunga Kiki Bertens kwenye mchezo wake wa nusu fainali.

Mchezo wa leo utakuwa ni wanne kwa wanadada hawa kukutana. Kwenye michezo mitatu iliyopita Barty ameshinda mara mbili na Osaka ameshinda mara moja. 

Osaka akishinda mchezo wa leo atakuwa amesawizisha idadi ya vipigoi alivyopata kutoka kwa Muaustralia huyo lakini kama atakubali kufungwa basi atakuwa kibonde wa Barty.

Kwenye fainali ya wanaume napo kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka ambapo Stefanos Tsitipas atamenyana dhidi ya Dominic Thiem.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya