China Open: Naomi Osaka Amemkalisha Bianca Andreescu Na Kutinga Nusu Fainali

5th October 2019

BEIJING, China -Mwanadada Naomi Osaka amefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya China Open baada ya kumdhibiti Bianca Andreescu kwenye mchezo mkali wa robo fainali.

Naomi Osaka
Naomi Osaka
SUMMARY

Ushindi huo unamfanya Osaka, 21, sasa kukutana uso kwa uso dhidi ya bingwa mtetezi wa michuano hiyo Caroline Wozniacki kwenye mchezo wa nusu fainali.

Haukuwa ushindi rahisi kwa Osaka ambaye ilimbidi apindue meza kibabe baada ya kuwa anaongozwa kwenye seti za awali na Andreescu ambaye ni bingwa wa US Open.

Osaka ambaye ni mchezaji namba moja wa zamani ameshinda kwa seti 5-7 6-3 6-4 kwenye mchezo uliofanyika kwa takribani saa mbili.

Ushindi huo unamfanya Osaka, 21, sasa kukutana uso kwa uso dhidi ya bingwa mtetezi wa michuano hiyo Caroline Wozniacki kwenye mchezo wa nusu fainali.

Kwenye nusu fainali nyingine, Ashleigh Barty ambaye ni namba moja kwa ubora kwasasa atacheza na Kiki Bertens.

Kwa upande wa wanaume, Andy Murry amefungwa kwa seti 6-2 7-6 (7-3) na Dominic Thiem na kutupwa nje ya michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo, Thiem sasa atacheza na Karen Khachanov kwenye nusu fainali.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya