CECAFA Wanawake: Uganda Yaibugiza Djibouti Mabao 13-0

18th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Timu ya taifa ya Uganda wanawake imeanza vyema michuano ya Cecafa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 13-0 dhidi ya timu ya taifa ya Djibouti kwenye mchezo wa kundi B uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi Complex.

Uganda
Uganda
SUMMARY

Kwa matokeo hayo Uganda wanashikilia usukani wa kundi B wakiwashusha Kenya ambao nao kwenye mchezo wao uliochezwa mapema waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ethiopia.

Mshambuliaji Juliet Nalukenge ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa Djibouti yeye peke yake akipachika nyavuni mabao 5 huku Fazila Ikwaput akifunga mabao matatu.

Wengine waliofunga mabao kwenye mchezo huo ni Hasifah Nasuuna, Fauzia Najjemba ambao kila mmoja alifunga mabao mawili. Bao moja limefungwa na Zaina Namuleme na kukamilisha idadi hiyo.

Kwa matokeo hayo Uganda wanashikilia usukani wa kundi B wakiwashusha Kenya ambao nao kwenye mchezo wao uliochezwa mapema waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ethiopia.

Mabao ya Kenya kwenye mchezo huo yamefungwa kwenye kipindi cha pili dakika za jioni na Jentrix Shikangwa na Cythuia Musungu.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed