CECAFA Wanawake: Kilimanjaro Queens Watangulia Nusu Fainali

19th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Timu ya Kilimanjaro Queens jana imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Wanawake inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0

Kilimanjaro Queens
Kilimanjaro Queens
SUMMARY

Mabao ya wenyeji Kilimanjaro Queens katika mchezo wa leo yamefungwa na Donisia Daniel aliyefunga mabao mawili Asha Rashi ‘Mwalala’ alifunga bao moja na Mwanahamisi Omary alifunga bao moja na la nne kwenye mashindano hayo baada ya mechi iliyopita kufunga mabao matatu pake yake hat-trick.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Timu ya Kilimanjaro Queens jana imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Wanawake inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kundi A uliopigwa uwanja wa Azam Complex.

Ushindi huo unaifanya Kilimanjaro Queens kutoka kundi A, kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali huku ikisaliwa na mchezo mmoja mkononi kumaliza hatua ya makundi.

Burundi walitarajiwa kuisumbua Kilimanjaro, kufuatia kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Zanzibar Queens, lakini kadri mchezo ulivyoendelea walijikuta wakitepeta na kupokea kipigo hicho.

Mabao ya wenyeji Kilimanjaro Queens katika mchezo wa leo yamefungwa na Donisia Daniel aliyefunga mabao mawili Asha Rashi ‘Mwalala’ alifunga bao moja na Mwanahamisi Omary alifunga bao moja na la nne kwenye mashindano hayo baada ya mechi iliyopita kufunga mabao matatu pake yake hat-trick.

Katika mchezo wa mapema Zanzibar Queens waliendelea kuwa na mwenendo mbaya katika michuano hiyo baada ya kukubali kwa mara ya pili kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Sudan Kusini.


Kocha apangua kikosi

Katika hali ya kuwachanganya wapinzani kocha wa Kilimanjaro Queens, Bakari Shime alipangua kikosi chake ambacho kilianza mechi ya kwanza dhidi ya Sudan Kusini na kutumia wacheza wapya ambao hawafahamiki jambo ambalo liliwachanganya wapinzani wao Burundi.

Baadhi ya wachezaji waliopata nafasi ya kucheza leo ni nahodha Asha Rashid ‘Mwalala, Fatuma Salum, Tausi Abdallah  na Najiati Idrissa.

Kocha Burundi aitabiria ubingwa  Kilimanjaro Queens

Baada ya mchezo wa leo kumalizika kocha wa timu ya taifa ya Burundi Niyibimenya Daniella, ameitabiria ubingwa Kilimanjaro Queens, kufuatia kiwango bora wanachokionyesha na sapoti kubwa wanayopata kutoka kwa mashabiki wao.

Kocha huyo amesema pamoja na kuwaona katika mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan Kusini lakini leo timu hiyo imebadilika kabisa kiuchezaji kitu ambacho kiliwachanganya vijana wake na kujikuta wakilala kwa mabao hayo 4-0.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed