CECAFA Wanawake: Kenya Waisukuma Uganda Mdomoni Kwa Kilimanjaro Queens

22nd November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Timu ya taifa ya Kenya wanawake wamefinikiwa kumaliza vinara wa kundi B baada ya kuwafunga Uganda mabao 3-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kufunga pazia hatua ya makundi.

Uganda
Uganda
SUMMARY

Djbouti ndiyo timu pekee inayomaliza mechi zake kwenye kundi hilo huku wakiwa hawana pointi hata moja na pia wakiwa hawajafunga hata bao moja huku wao wakiwa wamefungwa mabao 33 ndani ya mechi 3.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa sasa Kenya watavaana na Burundi walioshika nafasi ya pili kundi A huku Uganda wakiumana na wenyeji Tanzania kwenye michezo ya nusu fainali itakayopigwa Jumamosi.

Mabao ya Kenya kwenye mchezo dhidi ya Uganda yamefungwa na Mercy Airo, Mwanalima Jereko na Jentrix Shikangwa.

Ethiopia Waambulia Alama 3

Baada ya kufungwa kwenye mechi zao zote mbili za awali kwenye kundi B hatimaye timu ya taifa ya Ethiopia nayo imeambua alama 3 baada ya kuwafunga Djibouti mabao 8-0 kwenye mchezo wa mapema.

Djbouti ndiyo timu pekee inayomaliza mechi zake kwenye kundi hilo huku wakiwa hawana pointi hata moja na pia wakiwa hawajafunga hata bao moja huku wao wakiwa wamefungwa mabao 33 ndani ya mechi 3.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed