CECAFA Challenge 2019: Kilimanjaro Queens Watoa Somo, Zanzibar Wakipigwa 'Mkono'

17th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Mabingwa watetezi wa michuano ya CECAFA Challenge kwa upande wa kina dada, timu ya taifa ya Tanzania 'Kilimanjaro Queens' wameianza michuano hiyo kwa kutoa somo kubwa

Kilimanjaro Queens
Kilimanjaro Queens
SUMMARY

Kumbuka Kilimanjaro Queens ndiyo mabingwa watetezi baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwenye michuano ya mwaka jana iliyofanyika nchini Kenya.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mabingwa watetezi wa michuano ya CECAFA Challenge kwa upande wa kina dada, timu ya taifa ya Tanzania 'Kilimanjaro Queens' wameianza michuano hiyo kwa kutoa somo kubwa baada ya kuwatandika timu ya Sudan Kusini kwa mabao 9-0.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni Mwanahamisi Omary "Gaucho" ambaye alifunga mabao matatu huku mabao mengine kwenye mchezo huo yakifungwa na Stumai Abdallah (mawili), Opa Clement (mawili), Donisia Daniel na Julitha Aminiel waliofunga bao moja kila mmoja.

Kama washambuliaji wa timu ya Kilamanjaro Queens wangekuwa makini zaidi wangeweza kufunga mabao mengi zaidi ya hayo.

Kumbuka Kilimanjaro Queens ndiyo mabingwa watetezi baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo kwenye michuano ya mwaka jana iliyofanyika nchini Kenya.

Zanzibar Wapigwa Mkono

Wakati Kilimanjaro Queens wakitaka, ndugu zao wa Zanzibar Queens wao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kupigwa mabao 5-0 na timu ya taifa ya Burundi.

Michuano hiyo inafanyika ndani ya jiji la Dar es salaam huku uwanja wa Azam Complex ndiyo ukitumika kwenye mechi zote.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed