Bundesliga: Bayern Munich Bila Kocha Mkuu Watauweza Mziki Wa Dortmund Leo? Bet Yako Unaweka Wapi?

9th November 2019

MUNICH, Ujerumani- Kwenye dimba la Allianz Arena leo kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Bayern Munich watakao waalika Borrusia Dortmund.

Roberto Lewandowski
Roberto Lewandowski
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.

Bofya HAPA kubet sasa

Mcheo huo utakuwa ni wa kusisimua kutokana na uwezo wa timu hizo mbili ndani ya soka la Ujerumani.

Munich wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kitakatifu cha mnbao 5-1 kutoka kwa Frankfurt wiki iliyopita, kipigo hicho kilisababisha hadi kocha Niko Kovac atupiwe virago vyake. Kwasasa timu ipo chini ya kocha wa muda Hansi Flick.

Mchezo baina ya timu hizo mara nyingi huwa ni ya kuvutia sana hasa zikikutana kwenye kipindi kama hiki ambapo mmoja anakuwa safi mwingine hovyo.

Watu wengi wanaweza kuwapa nafasi ya moja kwa moja Dortmund kutokana na fomu yao ya hivi sasa lakini mimi niwahakikishie tu mchezo utakuwa mgumu sana na timu yeyote inaweza kuondoka na ushindi.

Hiyo ni kutokana na historia yao ya muda wote pindi wanapokutana. Huu utakuwa ni mchezo wa 57 baina yao.

Kwenye michezo 56 iliyopita Bayern wameshinda mara 27 huku Dortmund wakishinda mara 16. Michezo 13 imekwisha kwa sare.

Dortmund wanakumbukumbu mbaya na uwanja wa Allienz Arena kwani kwa mara ya mwisho walipokwenda kucheza mchezo wa ligi walikutana na kipigo cha 5-0, hiyo ilikuwa ni April 6, 2019.

Hata hivyo msimu huu kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi, Dortmund aliweza kushinda kwa mabao 2-0.

Tatizo kubwa kwa Dortmund kwenye mchezo wa leo huenda likaanzia kwa mshambuliaji Robert Lewandowski ambaye amefunga kwenye michezo yote aliyoshuka dimbani msimu huu. 

Kwa lugha nyepesi ya mtaani unaweza kusema kuwa Dortmund wataingia uwanjani wakiwa tayari washafungwa bao moja au wao wakubali kazi ya kuwa timu ya kwanza kumsimamisha Mpoland huyo.

Ni swala la kusubiri na kuona je ni nani ataibuka na ushindi kwenye mchezo huo kipindi ambacho pia tunasubiri kuona kama kocha Arsene Wenger atakabidhiwa timu kama jinsi tetesi zinavyosema.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya