Baba Mwenye Gari: Yusuph Jackson Akabidhiwa Gari Lake Jipya Kutoka SportPesa Na Tigo

6th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Hatimaye mshindi wa Gari jipya kutoka SportPesa na Tigo, bwana Yusuph Jackson kutoka Serengeti amekabidhiwa zawadi yake.

Mshindi wa gari jipya, Yusuph Jackson (kulia) akikabidhiwa ufunguo wa gari lake jipya na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas mbele ya wana habari. Katikati ni Mtaalam wa kitengo cha huduma za Kidigitali wa Tigo, Bi Ikunda Ngowi (Picha na SportPesa News)

SUMMARY

"Leo nimefika hapa nimejionea kwa macho yangu na sasa naamini kabisa na pia nawashukuru SportPesa kwani ni kampuni ya kuaminika kabisa," alisema.

Jackson, 29, alitangazwa mshindi kwenye droo ya mwisho (6) ya promosheni ya Faidika Na Jero siku ya Jumatano ya Oktoba 30 ikiwa ni promosheni iliyodumu kwa siku 40 na kuwazawadia watanzania Simu janja aina ya Samsung A10s na gari jipya.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ufunguo wa gari lake jipya aina ya Renault KWID, Jackpot ambaye ni fundi mchomeleaji amesema ilimuwia vigumu kuamini kama kweli ameshinda mara baada ya kupigiwa simu ya ushindi ya Mkurugenzi wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas, siku ya droo.

Yusuph Jackson akiongea na wana habari

"Sikuamini kama kweli nimeshinda na hata mtu wa kwanza kumwambia naye hakuamini, lakini mpaka nilipoona kwenye taarifa ya habari ndio nikapata uhakika.

"Leo nimefika hapa nimejionea kwa macho yangu na sasa naamini kabisa na pia nawashukuru SportPesa kwani ni kampuni ya kuaminika kabisa," alisema.

Wa kwanza

Akizungumza mara baada ya kukabidhi funguo kwa mshindi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Ndugu Tarimba Abbas amesema kuwa SportPesa  imekuwa ikibadili maisha ya watanzania kila kukicha kupitia promosheni kabambe.

"Kama utaona sisi ndio kampuni ya kwanza ya michezo ya kubashiri ambayo tumetoa zawadi ya Gari.

"Na si hivyo tu, tangu tumeanza biashara hapa nchini, tumeshatoa Bajaji zaidi ya 220 kwa watanzania mbalimbali, hivyo utaona mbali na pesa ambazo watu wanajishindia kila siku kwenye kubashiri lakini bado wanaweza kushinda zawadi mbalimbali ambazo zinawabadilishia maisha," alifafanua.

Baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Renault Posta jijini Dar es Salaam, Magabe ataondoka kuelekea Serengeti na gari lake jipya akiongozana na timu nzima ya SportPesa News.

Endelea kufuatilia tovuti yetu au tembelea ukurasa wa INSTAGRAM au FACEBOOK wa SportPesaTanzania kwa maudhui ya kukata na shoka kuhusu mshindi na kujua jinsi gani familia yake imepokea ushindi huo.