Amekaa: Mwakinyo Amkalisha Mfilipino Kwa Pointi Uwanja Wa Uhuru

30th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Bondia Hassan Mwakinyo ambaye anadhaminiwa na kampuni bora kabisa ya michezo ya kubashiri ya SportPesa amefanikiwa kumfinyanga Mphilipino, Arnel Tinampay kwenye pambano la kimataifa la kirafiki

Hassan Mwakinyo
Hassan Mwakinyo
SUMMARY

Mbinu ya kushambulia kwa kushtukiza hasa walipokutana katikati ya ulingo ilionekana kumzidi kimo Mphilipino ambaye alilazimika kuwa anamfinya Mwakinyo kwenye kona ili yeye apate nafasi ya kushambulia kwa uhuru.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Bondia Hassan Mwakinyo ambaye anadhaminiwa na kampuni bora kabisa ya michezo ya kubashiri ya SportPesa amefanikiwa kumfinyanga Mphilipino, Arnel Tinampay kwenye pambano la kimataifa la kirafiki lililofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Kwenye pambano hilo la raundi 10, Mwakinyo ameshinda kwa pointi baada ya jaji wa kwanza kumpa alama 97-93, jaji wa pili 98-92 na jaji wa tatu akitoa alama 96-96.

Kwa matokeo hayo Mwakinyo ameendeleza rekodi yake ya kutoa vichapo kwa mabondi hasa kwenye mapambano ya kimataifa yaliyofanyika kwa miezi ya hivi karibuni.

Kama ilivyo kawaida ya mabondia wengi kutoka Uphilipino huwa wanapiga ngumi nyingi mfululizo tena kwa haraka sana. 

Hivyo ndivyo Tinampay alivyofanya kwenye muda mwingi wa mchezo alionekana kutaka kuwa na kasi ya hali ya juu na kumzidi maarifa Mwakinyo.

Hata hivyo Mwakinyo alionekana kutotetereka sana na mashambulizi hayo kwani alijilinda vizuri lakini pia alishambulia kwa kushtukiza kila alipopata nafasi ya kufanya hivyo.

Mbinu ya kushambulia kwa kushtukiza hasa walipokutana katikati ya ulingo ilionekana kumzidi kimo Mphilipino ambaye alilazimika kuwa anamfinya Mwakinyo kwenye kona ili yeye apate nafasi ya kushambulia kwa uhuru.

Mwakinyo alionesha uhai sana wakurusha makombora yenye macho kwenye raundi za 3, 5, 7 na 9 ambapo kama si uvimulivu wa Tinampay basi huenda pambano hilo lingeisha kwa KO kabla ya raundi ya 10.

Mapambano Ya Utangulizi

Kwenye mapambano ya utangulizi tumeshuhudia burudani ya aina yake ambapo Mfaume Mfaume alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Keisi Ally.

Pia Twaha Kiduku raia wa Tanzania amefanikiwa kumpiga France Ramabolu raia wa Afrika Kusini kwa pointi.

Naye Meshack Mwankemwa amefanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Adam Yusuph mabondia wote wakiwa ni watanzania.

Said Chino amempiga Mohamed Bakari kwa pointi nao wote wakiwa ni mabondia kutoka nchini Tanzania.

Salim Mjengo kutoka Tanga naye amempiga Loren Japhet wa Dar es salaam kwa pointi.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya