ATP: Rodger Federer Atinga Nusu Fainali Baada Ya Kumpasua Novak Djokovic

15th November 2019

LONDON, Uingereza- Ndoto za nyota wa tenesi Novak Djokovic kumaliza mwaka akiwa kama mchezaji namba moja kwa ubora duniani zimezimwa baada ya kufungwa na Rodger Federer na kutupwa nje ya michuano ya nane bora.

Federer
Federer
SUMMARY

Djokovic alikuwa anahitaji kupata ushindi ili avuke nusu fainali na wakati huo amuombee mabaya Rafael Nadal ambaye naye leo ana mchezo mgumu dhidi ya Stefanos Tsitsipas.

Wawili hao wanagombea nafasi ya kwanza kwa ubora duniani ambayo kwasasa inakaliwa na Nadal lakini kama Djokovic angefanya vizuri huku kinyume chake Nadal angefanya vibaya basi hadhi zao za ubora zingegeuka.

Kwenye mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo, Federer ambaye alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kumfunga Djokovic alifanikiwa kushinda kwa seti 6-4 6-3.

Kwasasa Federer anasubiri kukutana na mmoja kati ya Nadal au Tsitsipas wanaotokea kundi A kwenye hatua inayofuata ambayo ni ya nusu fainali.

Hata hivyo kama Alexander Zverev atashinda mchezo wa leo dhidi ya Daniil Medvedv basi safari ya Nadal nayo itakuwa imefika mwisho bila kujali amepata matokeo gani leo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya