ATP: Rafael Nadal Afufua Matumaini Ya Kutinga Nusu Fainali, Bingwa Mtetezi Apigwa

14th November 2019

LONDON, Uingereza -Mchezaji tenesi namba moja kwa ubora duniani upande wa wanaume Rafael Nadal amepambana kutoka nyuma na kufanikiwa kupata ushindi mbele ya Daniil Medvedev kwenye mchezo wa michuano ya nane bora.

Nadal
Nadal
SUMMARY

Nadal, 33 anashika nafasi ya kwanza kwa ubora lakini ataweza kuipoteza nafasi hiyo kwa Novak Djokovic kama atashindwa kufika walau nusu fainali ya michuano hii.

Ushindi huo unafufua matumaini ya Nadal kutinga nusu fainali baada ya kuanza michuano hii vibaya kwa kufungwa na Alexander Zverev siku mbili zilizopita.

Nadal amemfunga Medvedv kwa jumla ya seti 6-7 (3-7) 6-3 7-6 (7-4) na sasa atalazimika kumfunga Tsitsipas kwenye mchezo wa kesho Ijumaa ili aweze kutinga nusu fainali.

Mara baada ya kumfunga Medvedev, Nadal alikiri kabisa kuwa alikuwa na bahati sana kwenye mchezo huo na hadi kufanikiwa kupata ushindi.

Nadal, 33 anashika nafasi ya kwanza kwa ubora lakini ataweza kuipoteza nafasi hiyo kwa Novak Djokovic kama atashindwa kufika walau nusu fainali ya michuano hii.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo, bingwa mtetezi wa michuano hii Zverev amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa bwana mdogo Tsitsipas.

Tsitsipas ameshinda kwa jumla ya seti 6-3 6-2 na sasa atahitajika kufanya vizuri zaidi dhidi ya Nadal ili kutinga nusu fainali.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya