ATP: Rafael Nadal Aaga Mashindanoni Licha Ya Kumtandika Tsitsipas Lakini

16th November 2019

LONDON, Uingereza- Rafael Nadal ameaga mashindano ya nane bora licha ya kuibuka na ushindi dhidi ya Stefanos Tsitsipas kwenye mechi ya jana jioni.

Rafael Nadal
Rafael Nadal
SUMMARY

Kwa maana hiyo sheria iliyotumika kumtoa Nadal ni ile ya Head to Head ambapo wawili hao walipokutana kwenye mechi ya kwanza kabisa ndani ya kundi hilo, Nadal alifungwa na Zverev.

Nadal ameshinda kwa seti 6-7 (4-7) 6-4 7-5 lakini hata hivyo alikuwa akitegemea zaidi matokeo ya mchezo kati ya Alexander Zverev dhidi ya Daniil Medvedev.

Kama Zverev angeshindwa kumfunga Medvedev basi Nadal angeweza kufuzu hatua ya nusu fainali. Lakini ushindi wa Zverev dhidi ya Medvedev umemfanya kufikisha idadi ya ushindi mara mbili kama alivyofanya Nadal.

Kwa maana hiyo sheria iliyotumika kumtoa Nadal ni ile ya Head to Head ambapo wawili hao walipokutana kwenye mechi ya kwanza kabisa ndani ya kundi hilo, Nadal alifungwa na Zverev.

Matokeo hayo sasa yanafanya Zverev kusonga mbele na kukutana na Dominic Thiem kwenye hatua ya nusu fainali ambayo itaanza kupigwa leo usiku. Mchezo mwingine wa nusu fainali utakuwa ni kati ya Rodger Federer dhidi ya Tsitsipas.

Nadal licha kuwa ameshinda Grand Slams 19 lakini bado hajawahi kuonja ladha ya ubingwa wa ATP.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya