ATP: Dominic Thiem Amchakaza Novak Djokovic Na Kutinga Nusu Fainali

13th November 2019

LONDON, Uingereza- Siku mbili baada ya kumfunga Rodger Federer, Dominic Thiem ameendeleza ubabe wake dhidi ya vigogo baada ya kumtandika Novak Djokovic kwenye mchezo wa pili wa kundi A la michuano ya nane bora na kufanikiwa kutinga nusu fainali.

Djokovic
Djokovic
SUMMARY

"Ni aina ya mechi ambazo kwakweli siwezi kuzisahau, nimekaa ndani ya mchezo kwa muda mrefu, ni kitu kizuri sana kutoka nyuma alafu kuja kuibuka na ushindi," amesema Thiem mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

LONDON, Uingereza - Siku mbili baada ya kumfunga Rodger Federer, Dominic Thiem ameendeleza ubabe wake dhidi ya vigogo baada ya kumtandika Novak Djokovic kwenye mchezo wa pili wa kundi A la michuano ya nane bora na kufanikiwa kutinga nusu fainali.

Thiem ambaye ni raia wa Australia ameshinda kwa seti 6-7 (5-7) 6-3 7-6 (7-5) na kusonga mbele huku akiwaachi kisanga Federer na Djokovic ambao itawabidi kugombea nafasi moja iliyobaki ili kutinga hatua ya nuu fainali.

Federer ambaye alifungwa kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Thiem amefanikiwa kushinda dhidi ya Matteo Berrettin ambaye sasa anakuwa amepoteza michezo yake yote miwili kwenye kundi hilo.

Mchezo wa mwisho ambao utaamuwa ni nani aende nusu fainali kuungana na Thiem utakuwa ni Djokovic dhidi ya Federer na mshindi atasonge mbele huku wakati huo Thiem akiwa anakamilisha ratiba dhidi ya Berrettin.

"Ni aina ya mechi ambazo kwakweli siwezi kuzisahau, nimekaa ndani ya mchezo kwa muda mrefu, ni kitu kizuri sana kutoka nyuma alafu kuja kuibuka na ushindi," amesema Thiem mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya