ATP: Djokovic Aanza Kwa Ushindi Wakati Federer Akitepeta Mbele Ya Thiem

11th November 2019

LONDON, Uingereza -Novak Djokovic ameanza kwa kishindo michuano ya nane bora kwa kumfunga Matteo Berrettin kwa juma ya seti 6-2 6-1 kwenye mchezo wa kundi A.

Novak Djockovic
Novak Djockovic
SUMMARY

Kwenye kundi hilo baadaye tutashuhudia mchezo wa kukata na shoka ambapo sasa Djokovic akiwa na ushindi wake atakabiliana uso kwa uso na Federer.

LONDON, Uingereza -Novak Djokovic ameanza kwa kishindo michuano ya nane bora kwa kumfunga Matteo Berrettin kwa juma ya seti 6-2 6-1 kwenye mchezo wa kundi A.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo tumemshuhudia Rodger Federer akikubali kipigo cha seti 7-5 7-5 kutoka kwa Dominic Thiem.

Djokovic ambaye anakimbizia rekodi ya kufikisha mataji sita lakini pia amepania kumnyoa Rafael Nadal kileleni kwenye nafasi ya kwanza kwa ubora upande wa wanaume.

Kwenye kundi hilo baadaye tutashuhudia mchezo wa kukata na shoka ambapo sasa Djokovic akiwa na ushindi wake atakabiliana uso kwa uso na Federer.

Huo utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa miamba hao ambao mara ya mwisho walikutana mwezi Julai, 2018 kwenye fanali ya Wimbledon.

Djokovic atamfunika Nadal kwenye viwango vya ubora mapema wiki ijayo lakini itambidi kwanza afike fainali ya michuano hii.

Michuano ya ATP inashirikisha wachezaji nane wa nafasi za juu kwa ubora ambapo wanagawanywa kwenye makundi mawili. Washindi wawili wa mwanzo wa kila kundi wanaingia nusu fainali.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya