AFCON 2021: Tunisia Waipiku Stars Kileleni Kundi J Baada Ya Kuitandika Libya

16th November 2019

TUNIS, Tunisia- Timu ya taifa ya Tunisia imeanza vyema harakati zake za kusaka tiketi ya kushiriki Afcon 2021 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Libya kwenye mchezo wa kundi J.

Tunisia
Tunisia
SUMMARY

Timu hizo zote za kundi J zitashuka dimbani tena Novemba 19 kucheza michezo yao ya pili. Tanzania watakuwa nchini Tunisia kwa ajili ya kucheza dhidi ya Libya huku siku hiyo Tunisia watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Equatorial Guinea.

Saif- Eddine Khaoui na Wahbi Khazri wote walifunga mabao mawili kila mmoja na kuwafanya miamba hao wa soka kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi hilo.

Kwenye mchezo wa mapema wa kundi hilo, Tanzania walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea na kwasasa watalazimika kukaa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Timu hizo zote za kundi J zitashuka dimbani tena Novemba 19 kucheza michezo yao ya pili. Tanzania watakuwa nchini Tunisia kwa ajili ya kucheza dhidi ya Libya huku siku hiyo Tunisia watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Equatorial Guinea.

Kwenye mechi nyingine ambazo zimechezwa jana usiku zote ziliisha kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.

Mjini Bulawayo, Zimbabwe wakiwa na nyota wao kama vile Khama Billiat na Knowledge Musona walishindwa kuondoka na ushindi mbele ya Botswana baada ya dakika 90 kuisha kwa 0-0.

Nao Morocco chini ya kocha wao mpya, Vahid Halilhidzic wakiwa nyumbani kwenye mji wa Rabat wameshindwa kufungana na wageni wao Mauritania.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya