AFCON 2021: Taifa Stars Kwenye Vita Nyingine Ya Kundi J Dhidi Ya Libya Leo

19th November 2019

MONASTIR, Tunisia- Timu ya taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo ipo ugenini nchini Tunisia kukabiliana na Libya ikiwa ni mechi ya pili kwa timu zote mbili zilizopo Kundi J, kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021.

Taifa Stars
Taifa Stars
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi hii kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.

Bofya HAPA kubet kuanzia JERO

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Mustapha Ben Jannet , uliopo kwenye mji wa Monastir Tunisia.

Libya wanacheza mechi zao Tunisia kama eneo lao la nyumbani hii ni kutokana na machafuko ya nchini kwao.

Timu zinaingia kwenye mchezo wa leo zikiwa zimetoka kupokea matokeo ya aina mbili tofauti kwenye michezo yao iliyopita.

Wenyeji Libya wakiwaa ugenini walitandikwa 4-1 na Tunisia huku Tanzania wao wakianza kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Equatoria Guinea nyumbani.

Kocha wa Taifa Stars Etienne Ndayiragije, amekiri kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini anafurahi kuona vijana wake wapo fiti baada ya kufanya mazoezi mepesi kwa siku mbili ambazo wamekuwa kwenye mji huo.

Amesema pamoja na Libya kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao mchezo wa kwanza dhidi ya Tunisia lakini hawawezi kuwadharau bali watacheza kwa tahadhari huku wakijipanga kutumia mashambulizi ya kustukiza.

"Libya siyo timu mbaya licha ya kuwa wamefungw mabao mengi kwenye mechi ya kwanza"

"Mchezo wa kesho (leo) utakuwa mgumu na timu zote zimepania kupata alama ili kujiweka vizuri kwenye msimamo," amesema Ndayiragije.

Kati ya wachezaji waliotumika katika mechi iliyopita dhidi Guinea, leo Stars watalazimika kucheza bila ya Erasto Nyoni ambaye ana maumivu ya goti na hakusafiri kabisa na timu.

Rekodi Libya vs Tanzania

Katika historia ya mchezo wa soka Libya na Tanzania zinakutana kwa mara ya pili katika mashindano tofauti nje ya mataifa yao.

Mara ya kwanza ilikuwa kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya ambapo Libya walikuwa wageni waalikwa na walipangwa kundi B sambamba na Tanzania. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2017 na matokeo baada ya dakika 90 ilikuwa ni 0-0.

Katika viwango vya ubora vilivyotolewa na FIFA hivi karibuni Libya wameizidi Tanzania wakishika nafasi ya 103 wakati Tanzania wakiwa 133.

Rekodi ya Libya kwenye Afcon

Katika nchi nne za Afrika Kaskazini, Libya ndiyo taifa pekee ambalo halina mafanikio katika mchezo wa soka ukilinganisha na majirani zao Misri, Algeria na Morocco.

Libya imewahi kushiriki Afcon mara tatu na mafanikio makubwa kwao ni kumaliza nafasi ya pili kwenye fainali za 1982 ambapo walitinga fainali na kufungwa na Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1, katika dakika 120.

Mwaka 2006 na 2012 walifuzu kwenye michuano hiyo lakini walitolewa mapema katika hatua ya makundi.

Wachezaji Wao Nyota

Elhouni Hamdou- Huyu ni kiungo hatari wa Libya ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Tunisia kwenye klabu ya Esperance mabingwa watetezi wa taji la ligi ya mabingwa Afrika. Huyu ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi dhidi ya Tunisia mechi iliyopita.

Soula Mohamed- Huyu ni mshambuliaji hatari wa Libya ambaye anaichezea klabu ya Etoile do Sahel ya Tunisia anarekodi nzuri ya kufunga mabao katika mechi kadhaa alizoichezea timu ya taifa walinzi wa Taifa Stars wanapaswa kumchunga.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed