AFCON 2021: Mechi Tano Za Kufuzu Afcon Ambazo Hautakiwi Kuzikosa

13th November 2019

CAIRO, Misri -Safari ya kuanza kugombea tiketi ya kwenda kushiriki michuano ya mataifa Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon inaanza leo ambapo miamba mbalimbali ndani ya bara la Afrika itaanza kumenyana kuwania alama tatu muhimu.

Algeria
Algeria
SUMMARY

Siku ya Ijumaa mwakati Tanzania tupo uwanjani kupepetana na Guinea, majirani zetu Kenya watakuwa nchini Misri kuvaana na Mafarao ambao kwenye Afcon iliyopita walikuwa ni wenyeji.

CAIRO, Misri -Safari ya kuanza kugombea tiketi ya kwenda kushiriki michuano ya mataifa Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon inaanza leo ambapo miamba mbalimbali ndani ya bara la Afrika itaanza kumenyana kuwania alama tatu muhimu.

Timu ya taifa ya Tanzania itakuwa na vibarua viwili mbele ya Equaterial Guinea siku ya Ijumaa na kisha watawafuata Libya ugenini kwenye mchezo wa Novemba 19.

Mfumo utakaotumika mwaka huu ni kama ule uliotumika msimu uliopita wa michuano iliyofanyika Misri ambapo timu mbili za juu kutoka kwenye kila kundi zitapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja.

Kama Stars watafuzu itakuwa ni mara yao ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo mapema mwaka huu ambapo walishiriki Afcon iliyofanyika kule Misri.

Mengi yamezungumzwa na yataendelea kuzungumzwa kuhusu mechi mbili za Stars. Kwakuwa mechi zitakazochezwa ndani ya wiki moja hii ni nyingi, SportPesa News tumeona ni bora tukurahisishie maisha kwa kukueleza mechi ambazo utapaswa kuzifuatilia zaidi.

Ghana v Afrika Kusini 

Mchezo wa kundi C baina ya timu mbele zenye historia pana ya soka la Afrika. Ghana watakuwa wenyeji wa mechi hii ambayo inatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa ndani ya dimba la Cape Coast.

Ghana wamekuwa hawana shida kwenye kufuzu, mara zote wamekuwa wakifanya hivyo lakini ishu yao kubwa imekuwa ni katika kulibeba taji hilo. Hivyo hivyo kwa Afrika Kusini ambao wao licha ya kuonekana kuwa wanamaendeleo makubwa sana kwenye soka lakini wamekuwa wakisuasua sana upande wa Afcon. 

Cameroon v Cape Verde

Cameroon ndiyo timu pekee ambayo hadi sasa imeshafuzu kwenye michuano hiyo kwakuwa wao ndiyo wenyeji. Hata hivyo wamepangwa kwenye kundi F pamoja na timu za Rwanda, Msumbuji na Cape Verde kwa ajili ya kutoa changamoto.

Siku ya leo majira ya jioni watakuwa nyumbani wakicheza mechi ya kwanza dhidi ya Cape Verde. Mvuto kwenye mechi hiyo unasababishwa na aina ya wachezaji wanaokwenda kukutana uwanjani

Cameroon kama inavyojulikana tangu zamani imekuwa ikizalisha wachezaji wengi wanaocheza ulaya na hali hiyo pia ipo kwa Cape Verde ambao wachezaji wengi wanacheza mpira wao nje ya bara la Afrika.

Hiyo maana yake nini? Maana yake ni kwamba leo kutakuwa na soka la ufundi mkubwa baina ya timu hizo mbili na ndiyo maana nikakwambia hautakiwa kuikosa mechi hii.

Misri v Kenya

Siku ya Ijumaa mwakati Tanzania tupo uwanjani kupepetana na Guinea, majirani zetu Kenya watakuwa nchini Misri kuvaana na Mafarao ambao kwenye Afcon iliyopita walikuwa ni wenyeji.

Shughuli ya Mahomed Salah nadhani hakuna asiyeijua lakini pia kuna nyota wengine wengi ambao wanaunda kikosi cha Misri. Hivyo hivyo kwa upande wa Kenya ambao watakuwa wakiongozwa na nyota wao na nahodha Victor Wanyama.

Mechi hii ni moja kati ya mechi za kuvutia kuona ni jinsi gani, Kenya watasimama imara dhidi ya wababe hao wa Afrika na ikiwezekana waweze kufuzu tena kwa mara ya pili mfululizo.

Nigeria vs Benin

Leo kwenye kundi L kutakuwa na pambano kati ya Nigeria dhidi ya Benini. Ni pambano ambalo litajumuisha timui mbili zenye hadhi tofauti.

Nigeria wanajulikana kama moja kati ya mataifa bora kimpira Afrika lakini Benin wao hawana historia yoyete kubwa. Hata hivyo kiwango walichoonesha Benin kwenye Afcon iliyopita kilikuwa siyo cha kubeza na hivyo kufanya watu pengine watarajie mshtuko kwenye mechi ya leo itakayopigwa kwenye dimba la Akpabio International.

Unaambiwa sababu kubwa ya mechi hiyo kupelekwa huko ni kwakuwa Nigeria wamekuwa na rekodi nzuri sana ya kutopoteza mchezo hapo. Kwa lugha nyepesi unaweza kusema Benin wamepelekwa machinjioni.

Algeria vs Zambia 

Mabingwa watetezi wa Afcon, Algeria watakuwa nyumbani siku ya Alhamisi kuwaalika mabingwa wa mwaka 2012 timu ya Zambia. Moto wa Algeria kwasasa ndani ya bara la Afrika sio mdogo na watakuwa wakiongozwa kama kawaida na kina Riyad Mahrez.

Zambia watatumia mbinu zipi kuweza kukabiliana na wenyeji hawa ambao wamepania kuendeleza undava wao, ni jambao la kusubiri na kuona.        

Imeandaliwa na Raheem Mohamed