AFCON 2021: Mambo 5 Tuliyojifunza Mechi Ya Stars v Equatoria Guinea

16th November 2019

DAR ES SALAAM,Tanzania- Ushindi wa mabao 2-1, ulioipata Taifa Stars, hapo jana umeongeza matumaini ya mashabiki wengi wa soka kuiona timu hiyo ikishiriki kwa mara ya pili mfululizo Afcon za 2021.

Tanzania vs Equatorial Guinea
Tanzania vs Equatorial Guinea
SUMMARY

Tofauti na mechi nyingine za Stars zilizopita mechi ya jana mashabiki walijitokeza kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu zote timu yao.

Acha tusubiri na kuona lakini pointi tatu za jana zilikuwa na umuhimu mkubwa katika safari ya kuelekea Cameroon 2021 ambapo itakuwa ni mara ya tatu kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika.

Hapa chini Mtandao wa SportPesa News, unakuletea mambo matano tuliyojifunza katika mpambano huo wa jana kati ya Tanzania na Equatorial Guinea.

Wachezaji wa Stars kushindwa kusoma mbinu za wapinzani

Katika kipindi cha kwanza wachezaji wa Stars, walishindwa kuwasoma wapinzani wao Equatorial Guinea, ambao walitumia muda mwingi kuupozesha mchezo na kupoteza muda kwa kujiangusha na kuchelewa kupiga mipira ya adhabu hasa baada ya kupata bao la kuongoza.

Wachezaji wa Stars, hawakuonyesha kulibaini hilo waliendelea kucheza kwa kuwaiga wao huku wakikosa mbinu mbadala za kusawazisha na kuwafanya wapinzani mbinu zao kufanikiwa kipindi cha kwanza.

Maelewano ya mawinga na washambuliaji wakati

Katika mchezo wa jana hakukuwa na maelewano mazuri kati mawinga na washambuliaji wa kati ambao ni Mbwana Samatta na Simon Msuva.

Kutokana na hilo krosi nyingi zilipokuwa zikipigwa kipa wa Guinea alikuwa anazidaka au zinakuwa zinapita juu na kuwa faida kwa wapinzani kipindi cha pili kwa kiasi fulani walionekana kujirekebisha wakafanikiwa kufunga bao la kusawazisha.

Wachezaji hawakumsoma mwamuzi

Ilikua ni jambo la kushangaza sana jana timu mwenyeji kupata kadi sita za njano huku wapinzani wakilata tatu tu.

Hii imeonyesha kwamba mwamuzi wa mchezo huo hakuwa fair kwa wenyeji na maamuzi yake mengi yalionyesha kuwafaidisha wageni ambao walitumia muda mwingi kumdanganya kwa kujifanya wamechezewa rafu.

Vituo vingi

Nikweli mpira una njia zake ili kupata matokeo lakini baada ya jana kutanguliwa wachezaji wa Stars hawakutakiwa kupiga pasi nyingi tena wakiwa kwenye eneo lao sababu ilikuwa ni faida kwa Guinea.

Nyakati kama zile walitakiwa kutumia mipira mirefu eidha ipite juu au chini kwa ajili ya kutafuta ushindi na angalia walipojaribu kufanya hivyo dakika za mwishoni walifanikiwa kufunga bao la ushindi kwa shuti kali la Sure Boy.

Mashabiki waonyesha uzalendo

Tofauti na mechi nyingine za Stars zilizopita mechi ya jana mashabiki walijitokeza kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu zote timu yao.

Mashabiki hao walitumia kila hila ikiwemo kuwamulika usoni na vitochi wachezaji wa Equatorial Guinea ili kuhakikisha timu yao inapata ushindi na kweli walifanikiwa hongera kwao.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed