AFCON 2021: Emmanuel Okwi Aibeba Uganda, Meddie Kagere Mambo Bado Magumu Rwanda

18th November 2019

JINJA, Uganda- Timu ya taifa ya Uganda wamefanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye michuano ya kufuzu Afcon 2021 baada ya kuwafunga Malawi 2-0 kwenye mchezo wa kundi B nakupanda kileleni kwenye msimamo.

Emmanuel Okwi
Emmanuel Okwi
SUMMARY

Matokeo hayo yanawafanya Uganda kufikisha alama nne baada ya kuanza michuano hii kwa kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Burkina Faso ugenini kwenye mechi ya kwanza.

Mabao ya Emmanuel Okwi aliyefunga kipindi cha kwanza na Fahad Bayo kipindi cha pili yalitosha kabisa kufanikisha ushindi huo.

Matokeo hayo yanawafanya Uganda kufikisha alama nne baada ya kuanza michuano hii kwa kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Burkina Faso ugenini kwenye mechi ya kwanza.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo, Burkina Faso wamewafunga Sudan Kusini mabao 2-1 na wao kufikisha alama nne akama Uganda na hivyo kubaki kwenye nafasi ya pili kutokana na uwinano wa mabao.

Malawi ambao wao walianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini kwenye mechi ya kwanza wanashuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu huku Sudan Kusini wakibakibia kwenye mkia wa kundi hilo wakiwa hawana alama yoyote baada ya mechi mbili.

Rwanda Wamefungwa Tena

Timu ya taifa ya Rwanda wamejikuta kwenye wakati mgumu ndani ya kundi F baada ya kuruhusu kufungwa bao 1-0 nyumbani na timu ya taifa ya Cameroon.

Kipigo hicho kinakuwa ni cha pili mfululizo kwa timu hiyo ambayo sikuu tatu zilizopita walifungwa 2-0 na timu ya taifa ya Msumbuji.

Kwenye mchezo huo mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alicheza mwanzo hadi mwisho huku pia kiungo wa zamani wa Yanga na Simba, Haruna Niyonzima akiwa ni sehemu ya mchezo huo.

Bao pekee la Cameroon amabao ni wenyeji wa michuano ya Afcon 2021 limefungwa na Nicolas Ngamaleu.

Matokeo Mengine

Chad 0-2 Mali

Guinea 2-0 Namibia

Sudan Kusini 1-2 Burkina Faso

Uganda 2-0 Malawi

Afrika Kusini 1-0 Sudan

Gabon 2-1 Angola

Rwanda 0-1 Cameroon

Eswatini 1-4 Senegal

Congo-Brazaville 3-0 Guinea-Bissau

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya