AFCON 2021: Comoros Waishangaza Afrika Baada Ya Kuwalazimisha Sare Misri

19th November 2019

MORONI, Comoros- Baada ya kuwafunga Togo kwa mabao 3-1 ugenini kwenye mchezo uliopita wa kundi G, Comoros wameendelea na wimbi la matokeo ya kushtukiza ndani ya bara la Afrika hiyo jana wakiwalazimisha Misri sare ya 0-0.

Egypt
Egypt
SUMMARY

Misri wanakuwa wametoa droo yao ya pili mfululizo tangu kuanza kwa mechi za kufuzu kufuatia droo nyingine ya 1-1 waliyotoa dhidi ya Kenya kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Cairo wiki iliyopita.

Pia kulikuwa na matokeo ya sare kwenye mechi za Cape Verde dhidi ya Msumbuji, Kenya dhidi ya Togo na Gambia dhidi ya DR Congo.

Ghana wamefanikiwa kushinda mechi ya pili kati ya mbili walizocheza kwenye kundi lao lakini safari hii haikuwa rahisi hata kidogo kwani iliwabidi wapambane jihadi kuhakikisha wanapata 1-0 dhidi ya Sao Tome ambao walikuwa nyumbani.

Misri wanakuwa wametoa droo yao ya pili mfululizo tangu kuanza kwa mechi za kufuzu kufuatia droo nyingine ya 1-1 waliyotoa dhidi ya Kenya kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Cairo wiki iliyopita.

Mafarao ambao wamemkosa Mohamed Salah kwenye mechi zote mbili walianza vizuri mchezo huo huku Mahmoud Kahraba akigongesha mwamba baada ya dakika tisa tu kupita.

Dakika mbili baadaye Misri walipata nafasi nyingine nzuri ya wazi ambayo ilimlazimu kipa wa Comoros kudaka mpira aliyorudishiwa na mchezaji mwenzake na matokeo yake ikwa ni faualo ya ndani ya boksi ambao waliokoa.

Timu zote zilikuwa na nafasi ya kufunga mabao kwenye kipindi cha pili lakini hakuna aliyeweza kutulia na kuweka mpira wavuni.

Kenya Wabanwa Nyumbani

Kenya waliweza kuwabana Misri ugenini kwenye mechi ya kwanza na jana wakiwa nyumbani dhidi ya Togo watu walitegemea huenda wangefanya vizuri zaidi.

Hata hivyo wamejikuta wakibanwa na kulazimishwa sare ya 1-1. Johanna Omolo ambaye ni mzaliwa wa Ubelgiji ndiyo aliyewapa Harembee Stars bao la kuongoza kwenye dakika ya 35 kipindi cha kwanza baada ya kupiga shuti kali lililomzidi maarifa kipa wa Togo, Malcolm Barcola.

Togo waliweza kuchomoa bao hilo dakika ya 64 kipindi cha pili baada ya mpira mzuri wa kona uliochongwa kutoka upande wa kulia kutua vyema kwenye kichwa cha Hakim Ouro na kumshinda mlinda lango Ian Otieno.

Matokeo hayo yanamaana kuwa Comoros ndiyo vuiongozi wa kundi hilo kwasasa wakiwa na alama 4 huku Kenya na Misri wakiwa na alama mbili na mwisho kabisa wapo Togo wenye alama 1.

Gambia Wabanwa Nyumbani

Gambia wakiwa nyumbani iliwabidi watoke nyuma mara mbili kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wageni wao timu ya taifa ya DR Congo.

Cedric Bakambu alianza kufunga bao kwa upande wa wageni mapema kipindi cha kwanza lakini wenyeji walichomoa bao hilo kipindi cha pili kupitia kwa Pa Modou Jagne.

Zikiwa zimesalia dakika 15 mpira kuisha, Jackson Muleka aliwainua tena vitini mashabiki wa DR Congo kwa kufunga bao la pili. Hata hivyo Baboucarr Jobe aliwahakikishia wenyeji kwamba hawafungiki kwa kufunga bao safi la kuchomoa kwenye dakika za majeruhi.

Mabingwa Watetezi Wanapiga Tu

Baada ya ushindi wa 5-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Zambia, mabingwa watetezi wa michuano ya Afcon, Algeria jana wameendeleza ushindi kwenye mechi za makundi baada ya ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Botswana.

Mfungaji wa bao pekee la washindi limefungwa na Youcef Belaili.

Matokeo Kamili

Sao Tome 0-1 Ghana

Gambia 2-2 DR Congo

Cape Verde 2-2 Msumbuji

Comoros 0-0 Misri

Kenya 1-1 Togo

Botswana 0-1 Algeria

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya