Muda Wa Mikeka: Baada Ya Kupigwa 9-0 Soton Leo Uso Kwa Uso Na Man City Carabao Cup
29th October 2019
MANCHESTER, Uingereza -Michuano ya kombe la Carabao inaendelea wiki hii kwa siku mbili mfululizo, kivumbi kikianza siku ya leo ambapo mechi tano zinatarajia kupigwa.
Shinda MAMILIONI na GARI jipya!
Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI katika masoko kibao pamoja na GARI jipya kesho!
Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya ushindi
Mabingwa watetezi Mancheters City na Leicester City leo zitakuwa ni timu pekee zilizopo kwenye nne bora kushuka dimbani usiku wa leo.
Man City wao watakuwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad kuwakaribisha Southampton ambao wametoka kupigwa bao 9-0 na Leicester City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika Ijumaa iliyopita.
Leicester City kwa upande wao watajaribu kuhamisha fomu yao ya kwenye ligi kuja kwenye michuano hii ambapo leo watakuwa ugenini kukabiliana na Burton Alibion.
Mbali na mechi ya Man City dhidi ya Soton lakini kutakuwa na mechi nyingine ambayo itazihusisha timu za EPL tupu ambapo Everton watakuwa nyumbani kuwakaribisha Watford.
Kwa miaka mingi michuano hii imekuwa na msisimko wa aina yake na msisimko wenyewe huwa unatokana na aina ya matokeo ambayo mara nyingine huwa hayasadifu uhalisia.
Makocha wengi wa timu kubwa na nyingine ambazo zinashiriki EPL huwa wanatabia ya kupangua vikosi vyao na kuwapa nafasi vijana na wachezaji ambao huwa hawachezi mara kwa mara. Hiyo husababisha kukutana na upinzani mkali kutoka kwa timu za madaraja ya chini ambazo zenyewe zinapania kweli kweli.
Kumbuka kuwa kwenye hatua hii ya sasa hakuna sare yaani timu zikishindwa kufungana basi changamoto ya mikwaju ya penati inafuata hadi mmoja atoke.
Man City v Southampton
Man City wana fomu nzuri kwenye ligi wakiwa wameshinda mfululizo, wanakutana na Soton ambayo kwa kiasi fulani imepoteza muelekeao na hii ni baada ya kupigwa mabao 9-0 na Leicester City kwenye mchezo wa ligi.
Soton wao itawapasa kuingia kwenye mchezo huu kwa tahadhari kubwa hasa ukizingatia wikiendi wanakutana tena na Man City safari hii ikiwa ni kwenye mchezo wa ligi.
Man City wamefika hatua hii wakitoka kuwatoa Preston Nore End kwenye mzunguko uliopita wakati Soton wao waliwatoa Portsmouth.
Hizi ni mechi ambazo huwa zinatoa matokeo ya kikatili hasa kwa vigogo lakini sitegemei kama hii itakuwa ni siku mbaya kwa Man City.
Burton Albion v Leicester City
Leicester City chini ya kocha Brendan Rodgers watakuwa na tamaa ya kuendelea na fomu yao nzuri waliyo nayo kwenye ligi kuu ya Uingereza ambapo hadi sasa wao wanakalia nafasi ya tatu.
Wanakutana na mpinzani ambao kwa haraka unaweza ukasema ni mchekea lakini hata hivyo siyo kama wengi wanavyodhani.
Timu zote zina nafasi ya kuibuka na ushindi kulingana na sababu mbalimbali lakini Leicester City wana nafasi nzuri zaidi ya kutinga robo fainali.
Everton v Watford
Timu zote zipo katika wakati mgumu kwasasa lakini Watford wana hali mbaya zaidi. Hii ni kwasababu hadi sasa licha ya kuwa wapo kwenye hatua hii lakini hawajawahi kupata ushindi kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Kwenye mchezo wa leo nadhani utakuwa ni wa piga nikupige lakini Everton wakiwa nyumbani wanayo nafasi ya kufanya vizuri hasa ukizingatia kwenye mchezo wa ligi waliokutana msimu huu kwenye uwanja huo wa Godson Park, wenyeji walishinda kwa bao 1-0.
Ratiba Kamili Ya Leo
Everton v Watford
Man City v Southampton
Burton Albion v Leicester City
Oxford United v Sunderland
Crawley Town v Colchester
Imeandaliwa na Jerry Mlosa