Yanga Kunasa Nyota Watatu Wa Kimataifa Kwenye Dirisha Dogo La Usajili

17th October 2019 - by Adam Mbwana

DAR ES SALAAM, Tanzania- Uongozi wa Yanga umepania kulitumia vyema dirisha dogo la usajili kwa kusajili nyota wakimataifa watatu watakaoirudisha timu hiyo kwenye makali yake.

Mwinyi Zahera
SUMMARY

Aidha Dk. Msolla amesema kutokana na usajili wanaotarajia kuufanya watalazimika kuwatoa kwa mkopo au kuwauza baadhi ya wachezaji ili kutoa nafasi za kuweza kusajili.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kusajiliwa ni mshambuliaji hatari wa Rayon Sports ambae ni raia wa Ghana, Michael Sarpong mwingine ni kiungo mkongwe Haruna Niyonzima na beki wa kushoto Erick Rutanga.

Akizungumza na SportPesa News, Mwenyekiti wa timu hiyo Dk. Mshindo Msolla, amesema wamejipanga kuhakikisha wanakamilisha usajili huo ili kukiimarisha kikosi chao kiweze kufanya vizuri.

“Tumegundua usajili wetu tuliofanya kwenye dirisha kubwa hakututosheleza bado tuna mapungufu ndiyo tunataka kuziba kwenye dirisha dogo ili tuweze kurudi kwenye mbio za ubingwa msimu huu,” amesema Dk. Msolla.

Wamepanga kumwongeza Sarpong, kutokana na mapungufu waliyokuwa nayo kwenye ushambuliaji na mchezaji huyo anarekodi nzuri msimu uliopita ameifungia timu yake mabao 22 kwenye michuano yote.

Aidha Dk. Msolla amesema kutokana na usajili wanaotarajia kuufanya watalazimika kuwatoa kwa mkopo au kuwauza baadhi ya wachezaji ili kutoa nafasi za kuweza kusajili.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed