UEFA: Hizi Hapa Rekodi Za KRC Genk Ya Samatta Dhidi Ya Timu Za Uingereza
23rd October 2019
GENK, Ubelgiji- Leo majira ya usiku kwenye runinga zetu tutapaa nafasi ya kushuhudia moja kati ya matukio adimu sana kwa Watanzania.
Shinda MAMILIONI na GARI jipya!
Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi hii kali na nyingine kibao kupitia SportPesa uweze kujishindia donge nono katika masoko kibao leo.
Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya kushinda GARI jipyaaa.
Tukio hilo si lingine bali ni kumshuhudia Mtanzania mwenzetu, Mbwana Ally Samatta akituwakilisha kwenye michuano mikubwa kabisa ya vilabu barani ulaya na naweza kusema ni duniani kwa ujumla pale timu yake ya KRC Genk itakaposhuka dimbani kuwaalika Liverpool.
Ni tukio adimu si kwa kuwa ni mara ya kwanza Samatta anacheza kwenye michuano hiyo, laa hasha! ameshafanya hivyo mara mbili pale aliposhuka dimbani kucheza dhidi ya RB Solzburg na dhidi ya Napoli.
Hata hivyo mara hii itakuwa ni tukio zuri sana kwakuwa kwanza anakwenda kucheza dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo. Hiyo tu inatosha kusema leo anakwenda kukutana na timu bora kwa sasa Ulaya na duniani lakini si hivyo tu bali anakwenda kukutana dhidi ya wachezaji nyota sana ulimwenguni.
Beki bora wa dunia kwasasa bila ubishi ni Virgil van Dijk lakini pia unapotaja washambuliaji bora wanaotisha kama njaa huwezi kuwaacha Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino ambao wote kwa pamoja wamingia kwenye 30 bora ya kinyang'anyiro cha tuzo ya Ballon d Or.
Nadhani hata kufikia hapa utakuwa umenielewa nini ninachomaanisha. Kikubwa ni kwamba leo Samatta atashea uwanja mmoja na nyota hao na hilo siyo tukio dogo hata kidogo kwake na hata sisi Watanzania ambao tupo nyuma yake tukimshangilia na kumuombea dua afanye vizuri.
Samatta vs Van Dijk
Hili ndiyo jambo ambalo kila mmoja wetu kati ya watanzania zaidi ya milioni 50 tumekuwa tukijiuliza na kulitafakari.
Je ni vipi Samatta ataweza kuwa chini ya ulinzi wa Van Dijk beki ambaye ameonekana kuwa na kiwango cha hali ya juu kwasasa duniani.
Tunajua makeke ya Samatta pindi anapokuwa uwanjani. Ni mzuri kwenye kasi lakini pia amekuwa na tabia ya kupiga mashuti na hata kufunga sana mipira ya kichwa.
Hata hivyo ni swali ambalo itabidi majibu yake tuyapate ndani ya dakika 90 ili kujua ni vipi nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania atajichekecha kuweza kumfanya Van Dijk kuonekana nyanya mbele yake kama vile Takumi Minamino wa RB Solzburg.
KRC Genk vs Timu Za Uingereza
Hii ni mechi ya kwanza kwa Genk kukutana na Liverpool kwenye mechi za ushindani.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Genk kucheza na timu kutokana nchini Uingereza. Mara ya mwisho kwa Genk kukutana na timu kutoka Uingereza ilikuwa ni msimu wa 2011-12 ambapo walikutana na Chelsea na waliweza kuwabana kwa sare ya 1-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani kabla ya kwenda kupigwa 5-0 darajani. Hiyo ilikuwa ni kwenye hatua ya makundi.
Liverpool wanarekodi ya kushinda mechi zote tano walizokutana na timu kutoka Ubelgiji tena ushindi kwenye mechi tano hizo wameupata bila kuruhusu bao hata moja.
Timu za Uingereza hazijawahi kufungwa kwenye michezo 14 iliyopita ya michuano ya ligi ya mabingwa na timu kutoka Ubelgiji, wameshinda mechi 12 na kutoa droo mechi 2.
Timu ya mwisho kufungwa kutoka Uingereza ilikuwa ni Manchester United mwaka 2000 ilipofungwa na Anderlecht
Shinda MAMILIONI na GARI jipya!
Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi hii kali na nyingine kibao kupitia SportPesa uweze kujishindia donge nono katika masoko kibao leo.
Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya kushinda GARI jipyaaa.
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya