Mida Ya Kubeti: Fuatilia Dondoo Za Mechi Za Leo, Top Six Wote Wakijitupa Dimbani
2nd November 2019
MANCHESTER, Uingereza- Kivumbi cha Ligi kuu ya Uingereza mzunguko wa 11 kinaendelea leo ambapo takribani viwanja nane nyasi zake zitawaka moto.
Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?
Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.
Bofya HAPA kubet kuanzia JERO tu uingie kwenye droo ya ushindi
Mchezo wa mapema zaidi utakuwa ni kati ya Bournemouth ambao watakuwa nyumbani kuwakaribisha Man United huku mechi ya mwisho itashuhudiwa Watford ambao hawajashinda mechi hata moja msimu huu wakiwaalika Chelsea.
SportPesa News inarahisisha maisha kwa wazee wa mikeka kwa kuweka baadhi ya dondoo muhimu ili mdau kujua ni sehemu gani ya kuweka bashiri yako.
Bournemouth v Man United
Timu hizo kwenye mechi ya leo zinakutana kwa mara ya tisa. Kwenye mara nane zilizopita Man United wamekuwa wababe zaidi wakishinda mara sita, wakifungwa mara moja na sare baina ya miamba hao ni moja tu.
Bournemout wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kama hivi leo wamefungwa mara tatu na wao wakishinda mara moja tu.
Mechi tano za mwisho baina yao Man United wameshinda mechi 4, mbili nyumbani na mbili ugenini huku mechi moja ikiisha kwa sare ambayo ilifanyika Old Traford.
Fomu ya timu zote mbili kwasasa kwenye ligi unaweza kusema kuwa Bournemouth wapo vizuri zaidi ya Man United baada ya wao kukusanya alama sita kwenye mechi zao za mwisho huku United wakiwa wamekusanya alama tano tu.
Timu hizo zinalingana kila kitu kwenye msimamo zikiwa zina 13 kila mmoja wakiwa wameshinda mechi 3, wamedroo mara nne na kufungwa mara 3.
Arsenal v Wolves
Moja kati ya mechi za kuvutia kwa siku ya leo. Wolves hawapo vizuri msimu huu lakini bado wamekuwa na kikosi kinachotisha hasa wanapocheza na timu kongwe. Msimu huu wamesshafanya uharibifu ndani ya Etihad wakichomoka na ushindi wa 2-0.
Leo watakuwa Uwanja wa Emirates wakicheza mchezo wao wa 11 dhidi ya Arsenal. Kwenye michezo 10 iliyopita Arsenal wameshinda mara 7 wamefungwa mara moja na sare ni mbili baina yao.
Ushindi wa Arsenal mwingi ameupata akiwa ugenini nyumbani kwa Wolves ambapo wameshinda mara 4 lakini kwenye uwanja wa leo ambapo ni nyumbani kwa Washika Bunduki wameshinda mara tatu tu.
Wolves hana rekodi ya kupata ushindi ndani ya dimba la Arsenal lakini wanakumbukumbu nzuri ya ushindi wa 3-1 wakati timu zilipokutana kwa mara ya mwisho msimu uliopita.
Mechi tano za mwisho, Arsenal wameshinda mara mbili, wamefungwa mara moja na sare mbili.
Fomu yao kwasasa, kwenye mechi tano za mwishoi Wolves wapo vizuri zaidi ya Arsenal wakiwa hawajapoteza mechi hata moja wakiwa na ushindi mara mbili na sare tatu.
Arsena wao mechi zao tano za mwisho wameshinda mara mbili, sare mbili na kipigo mara moja. Wolves wapo nafasi ya 12 wakati Arsenal nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.
Aston Villa v Liverpool
Siku mbili baada ya kupangwa kukutana kwenye kombe la Carabao timu hizo zinakibarua kingine wikiendi hii kucheza mchezo wa ligi ndani ya Villa Park.
Wanakwenda kucheza mchezo wa 49. Kwenye michezo 48 iliyopita Liverpool ni wababe zaidi wakiwa na rekodi bora mara mbili ya ile ya Villa.
Liverpool wamerokodi ushindi kwenye mechi 26 wakati Vila wakiwa na ushindi kwenye mechi 12.
Kitu cha kuvutia ni kwamba ushidi huo mara 12 kwa Villa umegawanyika mara mbili, yaani mechi sita wameshinda nyumbani na sita ugenini kama ilivyo kwa Liverpool ambapo ushindi wao mara 26 nao umegawanyika mara mbili, mechi 13 nyumbani na 13 ugenini. Sare baina yao ni 10.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ndani ya Villa Park ilikuwa ni 2015 ambapo Liverpool waliibuka na ushindi wa 6-0 wakiwa ugenini.
Mechi taono za mwisho pia zinambeba Liverpool kitakwimu akiwa na ushindi mara tatu, huku Villa wakishinda mara moja tu na sare 1.
Liverpool ni vinara wa EPL kwasasa na fomu yao ni nzuri balaa wakiwa wameshinda mechi nne za mwisho huku mchezo mmoja wakitoka sare. Villa wao wameshinda mara mbili, wamefungwa mara mbili na sare 1 kwenye mechi zao tano za mwisho.
Man City v Southampton
Siku takribani tatu tangu walipokutana uwanja wa Etihad kucheza mchezo wa Carabao, leo timu hizo zinakutana tena uwanjani hapo kwa ajili ya ligi kuu.
Southampton wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha 9-0 kutoka kwa Leicester City wiki iliyopita.
Wanakwenda Etihad sehemu ambayo siyo salama hata kidogo kwao kwani mara ya mwisho timu hizo zilipokutana hapo msimu uliopita, Soton walipigwa 6-1.
Hii ni mara ya 31 kwa timu hizo kukutana, kwenye mechi 30 zilizopita Man City wameshinda mara 17 huku Soton wakiwa na rekodi ya ushindi mara 6 tu na sare ni 7 baina yao.
Mechi zao tano za mwisho Soton wamefungwa mechi zote wakiruhusu mabao 15 huku ao wakiwa wamefunga mabao matatu tu.
Fomu yao kwenye ligi, Man City wameshinda mechi nne na wakifungwa mara moja kwenye mechi zao tano za mwisho wakati, Soton wakikusanya alama moja tu kwa kutoa sare huku mechi nne zote zikiisha kwa vipigo.
Watford v Chelsea
Watford wakiwa hawajashinda mechi yeyote msimu huu watashuka dimbani kusaka ushindi wao wa kwanza msimu huu dhidi ya vijana wa Frank Lampard, Chelsea.
Hiyo ni mechi ya 13 kwa timu hizo kukutana, mechi 12 zilizopita Chelsea wameshinda mara 8 huku Watford wakishinda mara 2. Sare ni mbili baina yao.
Mechi zao tano za mwisho kukutana Chelsea wameshinda mara nne huku Watford wakishinda mara moja hiyo ikiwa ni mwaka 2018.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kwamba hadi kufikia hatua hii, Watford ndiyo timu ambayo bado haijashinda. Hata hivyo kuna mabadiliko wameanza kuyaonesha kwenye mechi za hivi karibuni na dalili zinaonesha siku yeyote wataweza kupata alama tatu.
Kwenye mechi zao tano za mwisho wametoa sare mechi tatu mfululizo huku wakiwa wamefungwa mechi mbili, wakati Chelsea wana rekodi ya ushindi mara nne mfululizo huku wakiwa wamefungwa mechi moja tu.
Mechi Nyingine
Shefield v Burnley
West Ham v Newcastle
Brighton v Norwich City
Imeandaliwa na Jerry Mlosa