Ligi Kuu Bara: Bocco, Wawa Nje, Simba Wakiwakaribisha Mtibwa Sugar

13th September 2019 - by Adam Mbwana

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo Ijumaa watashuka dimba la Uhuru Dar es Salaam kuwakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa raundi ya pili wa ligi hiyo.

John Bocco akimiliki mpira mbele ya mchezoji wa Mtibwa Sugar
SUMMARY

Simba wanashuka dimbani siku ya leo kuumana na Mtibwa Sugar ukiwa ni mchezo wa pili wa Ligi ikiwa ni wiki mbili tangu watoke kuiadabisha JKT 3-1 mechi ya ufunguzi

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo Ijumaa watashuka dimba la Uhuru Dar es Salaam kuwakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa raundi ya pili wa ligi hiyo.

Timu hizo zinakutana zikiwa katika nafasi tofauti Simba wapo kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi tatu wakati Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 17 na haina pointi.

Huo utakuwa mchezo wa pili kwa timu zote Simba ambao ndio mabingwa watetezi mchezo wa kwanza waliifunga JKT Tanzania mabao 3-1, wakati Mtibwa ilipoteza ugenini kwa idadi kama hiyo ya mabao dhidi ya Lipuli FC.

Kwa matokeo hayo ni wazi mechi ya kesho itakuwa na ushindani mkali hasa kwa wageni Mtibwa Sugar ambao walipoteza mchezo wa kwanza.

Ni ushindi tu

Kuelekea mchezo huo kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi.

"Nimchezo mgumu kwa timu zote mbili kwasababu Mtibwa ni timu nzuri na ngumu lakini tumejipanga kuwakabili na kupata ushindi tukiwa nyumbani," amesema Aussems.

Kocha huyo amesema katika mchezo huo ataendelea kuikosa huduma ya nahodha wake John Bocco ambaye aliumia goti lakini ameshaanza mazoezi mepesi.

Wachezaji wengine watakao kosekana ni Pascal Wawa na mshambuliaji Wilkin da Silva na Rashid Juma.

Aussems amesema ataendelea kumpanga kipa Aishi Manula na beki Tairone ambae alionyesha kiwango ca juu huku nafasi ya ushambuliaji akitarajia kuwaanzisha Meddie Kagere sambamba na Cletus Chama na Sharaf Al Shaboub.

Kwaupande wake kocha wa Mtibwa Sugar Zuber Katwila, amejitapa kuwa wamekuja Dar es Salaam akiwa na kikosi kamili lengo likiwa ni kupata pointi tatu.

Katwila amesema amewafuatilia kwa karibu wapinzani wao Simba na amejua mbinu za kutumia ili kupata ushindi.

Amesema kuelekea katika mchezo huo hakuna mchezaji atakaye mkosa wachezaji wote waliowaanda kwa ajili ya mechi ya Simba wapo fiti kwa ajili ya pambano hilo.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed