Kikapu: Stephen Curry Bado Ni Kinara Wa Mkwanja NBA, Lowry Atinga 5 Bora

9th October 2019 - by Adam Mbwana

TORONTO, Marekani -Mapema wiki zimetoka habari zinazomuhusu mchezaji wa Toronto Raptors, Kyle Lowry kukubaliana na timu yake kuongeza mkataba mnono ambao utamuwezesha kubaki kwenye mji wa Toronto hadi mwaka 2021.

Stephen Curry
SUMMARY

LeBron James naye hayupo mbali kwenye ishu za mkwanja kwani kila mwaka kwenye akaunti yake anaweka kibindoni kiasi cha dola 35,654, 150 ambazo ni sawa na shilingi 82,161,379,625 (Bilioni 82.1). Fedha anazolipwa LeBron ni sawa na zile za Cris Paul wa Houston Rockets.

Inaelezwa kuwa mlinzi huyo mkongwe ambaye ameisaidia timu yake kushinda taji la NBA msimu uliopita atakuwa anavuta kiasi cha dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa mwaka.

Ongezeko hilo la mshahara limemsogeza Lowry na kuangia hadi kwenye tano bora ya wachezaji wanaovuna fedha nyingi kwenye ligi ya NBA.

Mtandao wa SportPesa News umezama na kuibuka na orodha kamili ya wachezaji ambao wanavuta fedha nyingi zaidi NBA hadi kufikia mwisho wa msimu ulioisha.

Stephen Curry (Golden State Warriors)

Nyota wa mchezo huo ambaye watu wengine wanasema kuwa yeye ndiyo Lionel Messi wa mpira wa kikapu.

Ndani ya timu yake ya Golden State Warriors anavuta kiasi cha dola 37,457,154 amabazo ni sawa na shilingi 86,323,304,841 (Bilioni 86.3) kwa mwaka. Hela hizo ni mjumuiko wa mshahara pamoja na posho mbalimbali.

Russell Westbrook (Oklahoma City Thunder)

Staa huyo wa Oklahoma City Thunder anakalia nafasi ya pili kwa kuwa mchezaji mwenye mkataba mnono ndani ya NBA.

Kwa mwaka anavuna kiasi cha dola 35,665,000 ambazo ni sawa na shilingi 82,186,382,352 (Bilioni 82.1)

Cris Paul (Houston Rockects)

Houson Rockets nao hawapo nyuma katika ishu za kuwawezesha vijana wao ambapo kwa mwaka wanamlipa Cris Paul kiasi cha dola 35,654, 150 sawa na shilingi 82,161,379,625 (Bilioni 82.1) kwa mwaka.

LeBron James (Los Angeles Lakers)

LeBron James naye hayupo mbali kwenye ishu za mkwanja kwani kila mwaka kwenye akaunti yake anaweka kibindoni kiasi cha dola 35,654, 150 ambazo ni sawa na shilingi 82,161,379,625 (Bilioni 82.1). Fedha anazolipwa LeBron ni sawa na zile za Cris Paul wa Houston Rockets.

Kyle Lowry (Toronto Raptors)

Jina jipya ambalo limeingia ndani ya tano bora, hii ikiwa baada ya kukubali mkataba mpya ndani ya timu ya mabingwa hao wa NBA msimu uliopita.

Anatarajiwa kuvuna kiasi cha dola 32, 700, 000 ambazo ni sawa na shilingi 75,353,839,980 (Bilioni 75.3), hela hizo atakuwa anavuna kila mwaka.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya