Tetesi: Real Madrid Waandaa Paundi Milion 86 na James Rodriguez Ili Kumnasa Kante

16th October 2019

MADRID, Hispania -Klabu Ya Real Madrid imeandaa ofa ya paundi milioni 86 pamoja na kiungo mshambuliaji raia wa Colombia, James Rodriguez kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Chelsea, Ng'olo Kante

Ng'olo Kante
Ng'olo Kante
SUMMARY

Tayari Real Madrid wameshamsajili golikipa Thibaut Courtois na Eden Hazard kutoka Chelsea

MADRID, Hispania -Klabu Ya Real Madrid imeandaa ofa ya paundi milioni 86 pamoja na kiungo mshambuliaji raia wa Colombia, James Rodriguez kwa ajili ya kuwapa klabu ya Chelsea ili tu wapate saini ya kiungo mkabaji wa raia wa Ufaransa, Ng'olo Kante. (El Desmarque-in Spanish).

Kiungo raia wa Croatia na klabu ya Barcelona, Ivan Rakitic, 31, anafikiria kujiunga na klabu ya Juventus au Manchester United baada ya kupoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa wa Hispania wa msimu uliopita. (Marca)

Klabu ya Tottenham Hotspurs imeongeza juhudi za kumsaka kocha wa zamani Manchester United, Jose Mourinho kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusu hatima ya kocha wao wa sasa Mauricio Pochettino.  (Express). 

Manchester United wanatarajia kuwaachia kwa mkopo wachezaji wake makinda Angel Gomes, Tahit Chong na James Garner kwenye dirisha la usajili la mwezi wa Januari. (Mail).

Wakati huo huo Manchester United wanasidikika kuwa wanahitaji huduma ya mshambuliaji wa Juventus, Mario Mandzukic, 33, kipindi cha usajili wa Januari lakini wamempa onyo kwamba kwanza apunguze mahitaji yake mshahara. (ESPN).

Kocha wa Arsenal Unai Emery hategemei kuongeza mchezaji yeyote kwenye kikosi chake kipindi cha usajili wa Januari. (The Athletic).

Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Olivier Giroud, 33,  anajiandaa kuondoka kipindi cha Januari kama ataendelea kusugua benchi na tayri timu kadhaa zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake ambazo ni Inter Milani na Vancouver Whitecaps. (Sun).

Inter Milan wanampango wa kuongeza bei ya kiungo wao Lautaro Martinez, 22, ili kuwaziondoa mchezoni timu zinazomtaka ikiwemo Barcelona. Kiungo huyo kwasasa bei yake kwenye mkataba ni Paundi milioni 96. (Tuttosport, via Mail).

Imeandaliwa Na Badrudin Yahaya