Tetesi: Mesut Ozil Amesema Kuwa Hana Mpango Wa Kuondoka Arsenal

17th October 2019

LONDON, Uingereza- Kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil, 31, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka kwenye timu yake ya Arsenal hadi mkataba wake utakapofika mwisho mwaka 2021.

Mesut Ozil
Mesut Ozil
SUMMARY

Arsenal pia wanatajwa kuiulizia huduma ya kiungo wa Real Madrid, Lucas Vazquez, 28 kabla ya kufanya mpango wa kumsajili kipindi cha Januari. (El Desmarque).

Kocha wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri anatarajia kuwachukuwa mshambuliaji Mario Mandzukic, 33, na Emre Can, 25 kwenda nao Manchester United kama atapewa nafasi ya kumrithi Ole Gunnar Solskjaer. (Express).

Manchester United wapo tayari kumuachia kiungo wao Paul Pogba, 26 kwenda Real Madrid kama wao watepewa kiungo Toni Kroos, 29. (Bild).

Chelsea wametajwa kuwa ndiyo timu yenye nidhamu mbovu kuliko zote kwenye ligi kuu ya Uingereza wakiwa na rekodi ya wachezaji wake kupata kadi nyingi tangu mwaka 19992. (Star).

Tottenham Hotspurs wanampango wa kumchukuwa kiungo wa Real Madrid, Isco kama watampoteza kiungo wao raia wa Denmark, Christian  Eriksen kwenye dirisha la usajili la Januari. (Express).

Arsenal pia wanatajwa kuiulizia huduma ya kiungo wa Real Madrid, Lucas Vazquez, 28 kabla ya kufanya mpango wa kumsajili kipindi cha Januari. (El Desmarque).

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya