Tetesi: Kisa Barcelona Aubameyang Amegoma Kuongeza Mkataba Mpya Arsenal

21st November 2019

LONDON, Uingereza- Nyota wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, 30, amegoma kuongeza mkataba mpya na Arsenal kwa sababu anasubiri ofa kutoka Barcelona. (Mirror).

Aubameyang
Aubameyang
SUMMARY

Jose Mourinho atajaribu kumrejesha nyota wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, na amekuwa akivutiwa na nyota huyo tangu akiwa Man United. (AS - in Spanish).

Mourinho Kuwavuta Bale, Fernandez

Jose Mourinho atajaribu kumrejesha nyota wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, na amekuwa akivutiwa na nyota huyo tangu akiwa Man United. (AS - in Spanish).

Wakati huo huo, Mourinho anamuwinda nyota wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, 25, pamoja na mlinzi wa kati wa Benfica Mreno Ruben Dias, 22, kadhalika  na kiungo wa Manchester United MSerbia Nemanja Matic, 31. (Independent)

Arsenal, Barcelona, Munich Kugeukia Kwa Pochettino?

Nyota wa zamani wa Arsenal mlinzi Martin Keown amesema Washika Bunduki wanabidi kumfikiria kocha wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino. (Mail).

Nalo gazeti la The Sun limeripoti kuwa Barcelona na Bayern Munich wapo tayari kumchukua Mauricio Pochettino.

Dzeko kurudi EPL

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumnasa nyota wa zamani wa Man City, Edin Dzeko, 33, katika dirisha la mwezi Januari.

Maddison Kuongeza Mkataba Mpya

Kiungo wa England James Maddison,22, ana mpango wa kusaini mkataba mpya na Leicester City licha ya kwamba amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United (Manchester Evening News).

Zlatan Huyooo AC Milan

Wakala wa Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola yupo kwenye mazungumzo na AC Milan kwa ajili ya kumrejesha nyota huyo wa Sweden kwa wababe hao wa zamani wa Italia . (Corriere dello Sport - in Italian).

Mbappe Atakiwa Ndani Ya Turin

Juventus watajaribu kumshawishi mshambuliaji kinda wa Ufaransa na klabu ya PSG, Kylian Mbappe, 20, kuipiga chini Real Madrid na kujiunga nao. (Tuttosport, via Sky Sports).

Conte Anamtaka Tena Giroud Italia

Inter Milan wanapanga kumg'oa mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kupoteza nafasi chini ya kocha Frank Lampard. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)

Imeandaliwa na Jerry Mlosa