Rais Wa Soka Bulgaria Ajiuzulu Baada Ya Kushindwa Kudhibiti Ubaguzi

16th October 2019

SOFIA, Bulgaria- Rais wa shirikisho la soka la Bulgaria, Borislav Mihaylov amejiuzulu nafasi hiyo leo kufuatia mashabiki wa timu yao ya Taifa kuwafanyia ubaguzi wachezaji weusi wa England katika mechi ya jana ya kufuzu Euro 2020.

Bugaria fans
Bugaria fans
SUMMARY

Mechi hiyo ambayo ilichezwa mjini Sofia nchini Bulgaria, England ikishinda kwa goli 6-0, ilisimama mara mbili kwenye kipindi cha kwanza kufuatia kelele za ubaguzi walizokuwa wakifanyiwa wachezaji wenye ngozi nyeusi wa England.

Mihaylov amejiuzulu baada ya waziri mkuu wa Bulgaria, Boyko Borissov kumtaka achukue hatua hiyo kwa madai ya kushindwa kusimamia nidhamu ya soka nchini humo.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa mjini Sofia nchini Bulgaria, England ikishinda kwa goli 6-0, ilisimama mara mbili kwenye kipindi cha kwanza kufuatia kelele za ubaguzi walizokuwa wakifanyiwa wachezaji wenye ngozi nyeusi wa England.

"Baada ya matokeo ya aibu tuliyopata jana kama taifa, naagiza kukata uhusiano uliopo baina ya serikali na BFU ikihusisha pia kusitisha malipo ya fedha hadi pale Borislav Mihaylov atakapoondoka madarakani," imesomeka taarifa ya waziri mkuu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya