Pre-Season: Giannis Antetokounmpo Afanya Balaa Bucks Wakiwagaragaza Uttah Jazz

10th October 2019

MILWAUKEE, Marekani -Timu ya mpira wa kikapu ya Milwaukee Bucks imeendelea kuwasha moto kwenye michezo yake ya kirafiki ili kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu wa NBA

Giannis Antetokounmpo
Giannis Antetokounmpo
SUMMARY

Habari ambayo siyo nzuri kwa mashabiki wa Bucks ni moja tu ambapo mlinzi wao Eric Bledsoe alilazimika kutomaliza mchezo kutokana na majeraha lakini bado haijajulika ni majeraha ya kiwango gani.

MILWAUKEE, Marekani -Timu ya mpira wa kikapu ya Milwaukee Bucks imeendelea kuwasha moto kwenye michezo yake ya kirafiki ili kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu wa NBA ambapo usiku wa kuamkia leo wamewagaragaza Utah Jazz kwa jumla ya vikapu 133-99.

Kwenye mchezo huo nyota alikuwa ni kijana wa Kigiriki, Giannis Antetokounmpo ambaye amefunga vikapu 22, assist 20 na kufanya rebound 4 ndani ya dakika 20.

Kama umesahau nikukumbushe tu kuwa Antetokounmpo ndiye MVP (mchezaji bora wa msimu) wa NBA msimu uliopita.

Mchezaji mwengine aliyefanya kazi nzuri kwa upande wa Bucks kwenye mchezo huo ni Brook Lopez na Khris Middleton ambapo kila mmoja alifunga vikapu 14.

Habari ambayo siyo nzuri kwa mashabiki wa Bucks ni moja tu ambapo mlinzi wao Eric Bledsoe alilazimika kutomaliza mchezo kutokana na majeraha lakini bado haijajulika ni majeraha ya kiwango gani.

Msimu wa ligi ya kikapu Marekani NBA unatarajia kuanza Oktoba 22, mwaka huu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya