Nyota Wa Wiki: Kyrie Irving Ana Kila Sababu Ya Kuwa Nyota Wa Wiki Wa NBA

29th October 2019

BOSTON, Marekani -Ikiwa ni takribani wiki moja tangu kuanza kwa vuta ni kuvute ya michuano ya ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani tayari nyota wameshaanza kuonesha maujuzi yao

Kyrie Irving
Kyrie Irving
SUMMARY

Kwenye mechi yake ya kwanza tu Irving alifanikiwa kupachika vikapu 50 kwenye mechi moja licha ya kuwa timu yake iliweza kupoteza mchezo kwa kufungwa na Minnesota Timberwolves kwa jumla ya vikapu 127-126.

BOSTON, Marekani -Ikiwa ni takribani wiki moja tangu kuanza kwa vuta ni kuvute ya michuano ya ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani tayari nyota wameshaanza kuonesha maujuzi yao na sisi kama SportPesa hatuachi kutambua mchango wao katika timu zao.

Kwenye wiki hii ya kwanza ya NBA mechi kadhaa zimechezwa huku baadhi ya timu zikiwa zimeshateremka dimbani mara mbili, tatu hata na zaidi.

Nyota wengi wameonesha uwezo wao, mfano MVP wa msimu uliopita Mgiriki, Giannis Antetokounmpo wa Mulwaukee Bucks amefanya balaa kubwa tangu kuanza kwa msimu huu lakini pia bila kumsahau Kawhi Leonard wa LA Clippers amekuwa na msaada mkubwa sana katika kuipandisha timu hiyo.

Hata hivyo linapokuja suala la kumtafuta mshindi basi mara nyingi huwa anapatikana mmmoja tu na hivyo kama SportPesa jicho letu la mchezaji bora wa wiki hii ya kwanza kwenye ligi ya NBA linaangukia kwa kijana Kyroe Irving.

Irving, 27 ambaye aliwahi kucheza timu za Cleveland Cavaliers na Boston Celtic msimu huu amejiunga na Brooklyn Nets akiungana na nyota wengine kama vile Kevin Durant aliyejiunga msimu huu akitokea Golden State Warriors. 

Kwenye mechi yake ya kwanza tu Irving alifanikiwa kupachika vikapu 50 kwenye mechi moja licha ya kuwa timu yake iliweza kupoteza mchezo kwa kufungwa na Minnesota Timberwolves kwa jumla ya vikapu 127-126.

Mbali na mchezo huo lakini Irving aliwaongoza wenzake kwenye mchezo wa pili kupata matokeo ya ushindi wa 113-109 dhidi ya New York Knicks ambapo yeye tena alifunga vikapu 26 ikiwa ni vingi kuliko mchezaji yeyote kwenye mchezo huo.

Hata mchezo wao wa leo ambapo wamefungwa tena na Memphis Grizzlies kwa jumla ya vikapu 134-133, Irving bado ameongoza kwenye upande wa kupachika vikapu akifunga 37.

Kwa ujumla kwenye mechi tatu amefunga vikapu 113 akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi mara moja na kufungwa kwenye michezo miwili kupitia muda wa nyongeza (At Over Time).

Kwa takwimu hizo ni wazi kabisa mchango wa Irving kwenye timu yake ni mkubwa mno na kwa kipindi cha siku saba hizi hauwezi kuufananisha na wachezaji wengine.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya