Mamilioni Yamerudi, Mourinho Ndani: Mambo Yatakuaje Kwenye Ligi Ya Kuu Ya Uingereza Wiki Hii?

22nd November 2019

LONDON, Uingereza -Ligi kuu ya Uingereza inarudi wikiendi hii, mmeshanisikia au niongeze sauti kidogo?

Jose Mourinho
Jose Mourinho
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI wikiendi hii?

Bet mechi kali kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi. Bofya HAPA kubet sasa

Yah! ni kweli inarudi tena inarudi ikiwa na kocha Jose Mourinho ambaye wikiendi hii tutamuona akiwaongoza Tottenham Hotspurs ugenini dhidi ya West Ham United.

Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili sasa mshike mshike huo unarudi na kama kawaida lazima kuna mambo ambayo lazima tutegemee kuyaona kama yanavyoainishwa kwenu na SportPesa News.

Mourinho Ndani Ya London Derby

Kipindi cha takribani mwaka mmoja wapenzi wa soka duniani tulikosa kumuona kocha Jose Mourinho kwenye kazi ya ukocha.

Hata hivyo wikiendi hii tutamuona kwa mara ya kwanza akiwaongoza Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya ugenini dhidi ya West Ham United.

Mechi hiyo ni ngumu kwa kuwa ni Derby ya London na hivyo huo ndiyo mtihani wa mwanzo kabisa wa kocha Mourinho kukabiliana nao kwenye mkataba wake wa miaka miwili na nusu ndani ya White Hart Lane.

Mechi Ya Kibabe

Kama ulikuwa unadhani kwamba EPL inarudi kinyonge basi futa hayo mawazo. Ligi inarudi kwa moto ule ule kama pale tulipoishia.

Siku ya Jumamosi tutapata fursa ya kushuhudia Manchester City ambao walifungwa kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Liverpool wakikutana na Chelsea ambao wameshinda mechi sita mfululizo za ligi kuu ya Uingereza.

Mechi hiyo itakuwa ni kali na ya kusisimua hasa ukiangalia msimamo wa ligi ambapo Chelsea wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 26 huku nyuma yao wakiwa City wenye alama 25.

Vibaru Vya Unai Emery na Solskjaer?

Kama kuna watu wanalaani kufutwa kazi kwa kocha Mauricia Pochettino basi ni makocha wa Mancester United na wa Arsenal.

Makocha hao wapo kwenye shinikizo kutokana na mwenendo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa wiki za hivi karibuni.

Kutimuliwa kazi kwa kwa Pochettino kunaongeza chachu kuelekea michezo yao ya wikiendi ambapo Arsenal watakuwa nyumbani dhidi ya Southampton huku Man United wakiwa ugenini dhidi ya Shefield.

Leicester City Kupunguza Kasi?

Leicester City imekuwa ni timu ya kuvutia sana msimu huu. Wanacheza soka safi na wanafunga mabao kwa kadiri wanavyotaka.

Wikiendi hii watakuwa ugenini dhidi ya Brigton timu ambayo imekuwa haitabiriki hasa kwenye ile michezo ya kibabe.

Watford Wamenza Kazi?

Ushindi wa 2-0 dhidi ya Norwich City kwenye mzunguko uliopita ulikuwa ndiyo ushindi wa kwanza wa Watford msimu huu.

Yaani jamaa walicheza mechi 11 bila kupata alama 3. Sasa wakiwa wanaingia kwenye mechi ya 13 ambapo watakuwa nyumbani dhidi ya Burnley ni swali la kujiuliza je wataendelea pale walipoishia au ile ilikuwa bahati tu dhidi ya ile timu dhaifu ya Norwich?

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya