Ligi Kuu Bara: Yanga Kuwapigisha Kwata JKT Tanzania Leo? Fuatilia Dondoo

22nd November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Ligi kuu soka Tanzania Bara inaendelea leo kwenye viwanja sita tofauti timu zikishuka kuwania alama 3.

Yanga
Yanga
SUMMARY

Yanga wameshinda mechi tatu mfululizo za ligi walizoshuka dimbani huku JKT Tanzania wakiwa na ushindi mmoja tu kwenye mechi zao tatu zilizopita.

Mechi ambayo itatolewa macho zaidi ni kati ya Yanga ambao watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Uhuru kupepetana na maafande wa JKT Tanzania.

Mchezo huo utakuwa ni wa sita kwa Yanga ambao kwenye michezo yao mitano iliyopita wamekusanya alama 10 wakiwa nafasi ya 15. JKT Tanzania wao wa[o nafasi ya 12 wakiwa na alama zao 12 baada ya kushuka dimbani mara 9.

Kuelekea mchezo wa leo taarifa iliyotoka ndani ya Yanga inasema kuwa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wanasumbuliwa na maumivu kwa siku za hivi karibuni wamepata nafuu na huenda wakawa ni sehemu ya mchezo huo.

Mohamed Issa "Banka", Ally Ally na Lamine Moro ni baadhi ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuwa kwneye kikosi cha kaimu kocha mkuu Charles Mkwasa.

Yanga wameshinda mechi tatu mfululizo za ligi walizoshuka dimbani huku JKT Tanzania wakiwa na ushindi mmoja tu kwenye mechi zao tatu zilizopita.

JKT Tanzania ilipanda daraja msimu uliopita na mechi mbili walizocheza na Yanga kwenye msimu huo waliambulia vipigo. Mechi ya kwanza walifungwa 3-0 na mechi ya pili walifungwa 1-0.

Mechi Nyingine

Tanzania Prison watakuwa kwenye uwanja wao wa Sokoine, Mbeya kuwakaribisha timu ya Mwadui kutoka Shinyanga. Kumbuka kuwa timu hizi ndiyo pekee ambazo zimeweza kuwasimamisha Simba msimu huu.

KMC bila kocha mkuu watakuwa ugenini dhidi ya Allience huku Kagera Sugar wao wakiwaalika Lipuli kwenye mechi itakayopigwa Kaitaba.

Ndanda baada ya kufungwa na Yanga kwenye mchezo uliopita wao watakuwa tena nyumbani kuwaalika Polisi Tanzania chini ya kocha wao Seleman Matola na Namungo watakuwa kwenye dimba la Kassim Majaliwa kuwaalika Wagosi Wakaya, Coastal Union.

Ratiba Kamili Leo

Namungo v Coastal Union

Ndanda v Polis Tanzania

Tanzania Prison v Mwadui

Kagera Sugar v Lipuli

Allience v KMC

Imeandaliwa na Raheem Mohamed