Ligi Kuu Bara: Tutegemee Nini Kwenye Mechi Za Ligi Wikiendi Hii?

22nd November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Mapumziko ya takribani wiki mbili bila kuwa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara yamefika tamati na sasa ni wazi kabisa tunaingia kwenye wikiendi nyingine ya mikimiki.

Mbeya City
Mbeya City
SUMMARY

Kabla ya kwenda mapumziko haya tulishuhudia Simba ambao ni vinara wa ligi tangu mwanzo wa msimu wakipunguzwa kasi na Tanzania Prison kwa kulazimishwa sare ya 0-0 na wakati huo ndugu zao Yanga wao wakipata alama 3 ugenini dhidi ya Ndanda kwenye mechi yao ya kwanza bila Mwinyi Zahera.

Kwa mujibu wa ratiba inaonesha kuwa mechi takribani 10 zitachezwa kati ya Ijumaa na  Jumamosi, hiyo ikiwa na maana timu zote zitashuka dimbani kwenye viwanja tofauti.

Kabla ya kwenda mapumziko haya tulishuhudia Simba ambao ni vinara wa ligi tangu mwanzo wa msimu wakipunguzwa kasi na Tanzania Prison kwa kulazimishwa sare ya 0-0 na wakati huo ndugu zao Yanga wao wakipata alama 3 ugenini dhidi ya Ndanda kwenye mechi yao ya kwanza bila Mwinyi Zahera.

Kuelekea michezo hii inayokuja mbele yetu, SportPesa News inakuletea mambo ambayo pengine tutatarajia kukutana nayo kwenye wikiendi hii.

Yanga Kuendeleza Wimbi La Ushindi?

Yanga hadi wanamtimua kocha Mwinyi Zahera tayari walikuwa wameshinda mechi mbili mfululizo ambazo ni dhidi ya Coastal Union na Mbao.

Alipokuja kocha mpya Charles Mkwasa naye akaendeleza walipoishia wenzake kwa kushinda mchezo wao wa mwishoi dhidi ya Ndanda ugenini.

Kumbuka kuwa mechi zote hizo tatu mfululizo wameshinda kwa bao 1-0 na leo hii wanakwenda kukutana na JKT Tanzania, swali ni je wataendeleza wimbi lao la ushindi na kufikia idadi ya mechi nne mfululizo.

Kagera Sugar Kuendelea Kuwapa Presha Simba?

Kagera Sugar ndiyo timu ambayo inaonekana kupania zaidi kuwakimbiza Simba kileleni. Tofauti yao ni alama mbili tu ingawa Simba wanapungufu ya mchezo mmoja kibindoni.

Hata hivyo Kagera Sugar atakuwa na mchezo wa nyumbani dhidi ya Lipuli siku ya leo Ijumaa na kama atashinda basi atazidi kuwa Simba presha kubwa pale kileleni.

Ruvu Shooting Kuendeleza Ubabe Kwa Wandewa?

Msimu huu Ruvu Shooting wamekuwa na matokeo ya kuvutia sana licha ya kuwa wamekuwa hawapo nafasi nzuri sana kwenye msimamo.

Ni kitu kikubwa sana kwa timu za daraja la Ruvu Shooting kuweza kuwafunga Yanga na Azam kwenye mechi hizi tu za mzunguko wa kwanza.

Siku ya Jumamosi watakuwa tena uwanjani kukabiliana na mndewa mwingine wa ligi timu ya Simba, na hapo ndiyo watu wengi itabidi tukodoe macho kuona kama moto wake dhidi ya timu kubwa utaendelea au vipi.

Mechi Ya Vibonde

Mbeya City watakuwa nyumbani kuwakaribisha wachovu wenzao Singida United. Mbeya City wao wapo nafasi ya 18 wakiwa na alama 8 huku Singida United wao wakiwa mkiani na alama nne.

Timu hizo zimekuwa zikipata tabu sana kupata alama zinapocheza na timu nyingine msimu huu lakini kwakuwa mechi hii wanacheza wenyewe kwa wenyewe basi tayari mmoja wao ana uhakika wa kupata alama au wote wakashea alama moja ya kujitunishia akaunti.

KMC Bila Kocha Mkuu

KMC wametimua kocha wiki mbili zilizopita na mchakato wa kumtafuta kocha mkuu bado unaendelea. 

Hata hivyo siku ya leo nao watalazimika kuingia uwanjani kucheza dhidi ya timu ya Allience kwenye mechi ya ugenini.

Mchezo huo hautakuwa mwepesi kwao hasa ukiangalia ubora wa Allience wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya