European Open: Andy Murray Ambwaga Stan Wawrinka Na Kushinda Taji Baada Ya Miaka 2

21st October 2019

LONDON, Uingereza- Mchezaji wa tenesi raia wa Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kushinda taji la European Open baada ya kumfunga Stan Wawrinka kwenye mchezo wa fainali uliofanyika Jumapili.

Andy Murray
Andy Murray
SUMMARY

Murray alifanyiwa upasuaji mapema mwezi Januari mwaka huu baada ya kuwa anasumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu na hii ni mechi yake ya saba kushiriki tangu alipopona.

Murray, 32, ameshinda kwa jumla ya seti 3-6 6-4 6-4 na kufanikiwa kushinda taji lake la kwanza baada ya miaka miwili.

Murray alifanyiwa upasuaji mapema mwezi Januari mwaka huu baada ya kuwa anasumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu na hii ni mechi yake ya saba kushiriki tangu alipopona.

Kwenye michuano mengine, wana dada Mswizi, Belinda Bencic na Mlatvia, Jelena Ostapenko wameshinda mataji tofauti kwenye michezo yao ya fainali waliyocheza jana.

Benci amemfunga Anastasia Pvlyuchenkova kwa jumla ya seti 3-6 6-1 6-1 kwenye mchezo wa fainali ya Russia Open na kushinda taji hilo.

Naye Ostapenko ameshinda Luxembourg Open baada ya kumfunga Julia Goerges kwenye mchezo wa fainali.

Ushindi huo umempa Ostapenko taji lake la kwanza tanu alipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2017.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya