EURO 2020: Uingereza Na Ureno Watatengeneza Njia Leo? Fuatilia Dondoo

14th November 2019

LONDON, Uingereza- Timu ya taifa ya Uingereza leo watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Wembley kuwakaribisha timu ya taifa ya Montenegro kwenye mchezo wa kundi A kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020.

Ronaldo
Ronaldo
SUMMARY

Bruno Fernandez, Bernaldo Silva, Joao Felix ni miongoni mwa vizazi ambavyo vimeingia vizuri kwenye timu kwa ajili ya kuwasaidia kina Cristiano Ronaldo ambao wanamalizia mpira wao kwasasa.

LONDON, Uingereza -Timu ya taifa ya Uingereza leo watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Wembley kuwakaribisha timu ya taifa ya Montenegro kwenye mchezo wa kundi A kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020.

Endapo timu ya Uingereza watafanikiwa kuibuka na ushindi leo basi watakuwa wamekata tiketi yao ya kufuzu kwenye michuano hiyo inayoshirikisha timu za taifa za bara la ulaya.

Mchezo wa leo ni wa marudiano baina ya timu hizo kweny kundi hil. Mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 25, mwaka huu Uingereza waliibuka na ushindi wa ugenini wa jumla ya mabao 5-1.

Kwasasa Uingereza wanaongoza kundi wakiwa na alama 15 baada ya kucheza michezo sita. Hiyo ikiwa na maana wamepoteza mchezo mmoja tu ambao ni dhidi ya Czech Republic. Nyuma ya Uingereza wapo Czech wenye alama 12 na Kosovo wenye alama 11.

Kwenye mchezo wa leo baina ya Uingereza dhidi ya Montenegro kocha Gareth Southgate tayari alishaweka wazi kuwa hatamtumia winga wake Raheem Sterling kutokana na utovu wa nidhamu aliounesha kambini siku ya Jumatatu.

Kabla ya mechi ya leo, timu hizi zimeshakutana mara 5 tangu mwaka 2010. Kwenye michezo hiyo, Uingereza wameshinda mara 2 huku michezo mitatu ikiisha kwa sare.

Montenegro wameshinda mchezo mmoja tu kwenye michezo mitano iliyopita ya timu ya taifa ambapo ilikuwa ni mwezi Septemba waliposhinda 2-1 dhidi ya Hungury mchezo wa kirafiki.

Uingereza wao wameshinda michezo minne kati ya mitano iliyopita na wamefungwa mchezo mmoja tu dhidi ya Czech kwenye hatua hii ya makundi.

Ureno v Lithuania

Kwenye uwanja wa Estadio Algarve leo usiku timu ya taifa ya Ureno watakuwa wakiwakaribisha timu ya taifa ya Lithuania.

Mchezo huo ni muhimu sana hasa kwa Ureno ambao hadi sasa bado hawajafuzu na nafasi kwenye kundi lao imebaki moja tu.

Ukraine tayari wamefuzu kwakuwa wana alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine. Kimbembe kimebaki kwa Ureno wenye alama 11 na Serbia wenye alama 10 na tmu zote zimebakiwa na michezo miwili. Ukiteleza umeachwa feli.

Ureno anahitaji kushinda leo na mchezo wao wa mwisho wiki ijao. Leo wanacheza na vibonde wa kundi Lithuania ambao hadi sasa wamekusanya alama moja tu kwenye mechi 7 wakiwa wanashika mkia.

Ureno kwa siku za hivi karibuni imekuwa ni moja kati ya timu nzuri zenye kuvutia kuzitazama kutokana na aina ya mpira wanaocheza lakini hata wachezaji walionao kwasasa.

Bruno Fernandez, Bernaldo Silva, Joao Felix ni miongoni mwa vizazi ambavyo vimeingia vizuri kwenye timu kwa ajili ya kuwasaidia kina Cristiano Ronaldo ambao wanamalizia mpira wao kwasasa.

Mabingwa hao watetezi wa Euro wana rekodi ya kushinda mechi zao nne kati ya tano zilizopita za timu ya taifa. Mechi pekee waliyofungwa ni ile ambayo walicheza kwa mara ya mwisho kabisa dhidi ya Ukraine ambapo walipoteza kwa 2-1.

Wanacheza na Lithuania leo ikiwa ni mara yao ya tatu tu kwenye maisha yao. Mara ya kwanza walicheza mwaka 2000 ambapo Ureno walishinda 5-1 na mara ya mwisho walicheza kwenye mchezo wa kwanza wa kundi hili ambapo pia walishinda 5-1.

Mechi Nyingine:

Czech v Kosovo

Uingereza v Montenegro

Ureno v Lithuania

Serbia v Luxembourg

Uturuki v Iceland

Albania v Andorra

Ufaransa v Moldova

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya