EPL: Mambo Matano Tuliyojifunza Ligi Kuu Ya Uingereza Mzunguko wa 12

11th November 2019

LONDON, Uingereza- Mizunguko 12 ya ligi kuu soka ya Uingereza imeshakatika na hali inaanza kuonesha si shwari kwa mabingwa watetezi Man City ambao jana wamekubali kichapo cha 3-1 kutoka kwa wapinzani wao wakubwa Liverpool.

Ole Gunnar Solskjaer
Ole Gunnar Solskjaer
SUMMARY

Wiki nyingine tena imepita huku kocha wa Spurs, Mauricia Pochettino kushindwa kupata ushindi. Unaambiwa anasaka ushindi wa kwanza kwenye ligi tangu mara ya mwisho waliposhinda mwezi Septemba.

LONDON, Uingereza -Mizunguko 12 ya ligi kuu soka ya Uingereza imeshakatika na hali inaanza kuonesha si shwari kwa mabingwa watetezi Man City ambao jana wamekubali kichapo cha 3-1 kutoka kwa wapinzani wao wakubwa Liverpool.

Kujua hayo na mengine makubwa yaliyojiri ndani ya wikiendi hiyo ya kibabe, ungana na SportPesa News ili tuongee kwa kina.

VAR Yatia Fora

Katika matukio ambayo yatazungumzwa sana kutokana na michezo ya wikiendi hii ni kitendo cha VAR kushindwa kuingilia kati na kutoa uamuzi kuhusu mipira miwili ambayo ilionekana dhahiri kugonga mkono wa mchezaji ndani ya boksi.

Hiyo ilikuwa ni kwenye mchezo wa Liverpool dhidi ya Man City ambapo mlinzi Alexander Anorld alionekana dhahiri kunawa mpira lakini mwamuzi Michal Oliver alifanya kama hakijatokea kitu kama vile ilivyofanya VAR.

Maisha Ya Unai na Pochettino

Wiki nyingine tena imepita huku kocha wa Spurs, Mauricia Pochettino kushindwa kupata ushindi. Unaambiwa anasaka ushindi wa kwanza kwenye ligi tangu mara ya mwisho waliposhinda mwezi Septemba.

Siyo yeye peke yake bali Unai Emery naye hali inazidi kuwa mbaya, hajashindi kwenye mechi tatu mfululizo za ligi lakini pia hii ni mechi tano mfululizo kwenye michuano yote bila ya ushindi.

Ingawa bado inaonekana kama wanapewa sapoti na viongozi wa juu lakini ni wazi kabisa makocha hao kwasasa wanamaisha magumu.

Watford Washinda

Ushindi wa 2-0 dhidi ya Norwich City siku ya Ijumaa ndiyo ulikuwa wa kwanza kwa Watford msimu huu tangu ulipoanza.

Ushindi huo umewafanya kufikisha alama 8 ndani ya mechi 12 na sasa wametoka mkiani mwa ligi wakisogea hadi nafasi ya 18 kwenye msimamo.

Man United Inaanza Kubadilika?

Ushindi wa 3-1 dhidi ya Brighton siku ya Jumapili umekuwa ni ushindi wa 5 kati ya mechi 6 walizocheza Man United kwenye michuano yote.

Ingawa ushindi huo siyo wa kwenye ligi kuu tu lakini hali ya kujiamini inaonekana kuanza kurudi ndani ya kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.

Liecester City, Chelsea Habari Nyingine

Wakati ligi inaanza hakuna aliyedhani kwamba hadi kufikia sasa Leicester City na Chelsea wangekuwa wanakimbizana na Liverpool kileleni.

Hata hivyo hiyo ndiyo hali ilivyo hivi sasa Leicester wakiwa nafasi ya pili na Chelsea nafasi ya tatu wote wakiwa na alama 26 alama 8 nyuma ya vinara Liverpool.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya