CECAFA Wanawake: Kilimanjaro Queens Yatinga Nusu Fainali Baada Ya Kuwafunga Zanzibar "Wiki"

21st November 2019

DAR ES SALAAM,Tanzania-Timu ya wanawake Tanzania Bara

Kilimanjaro Queens
Kilimanjaro Queens
SUMMARY

Kilimanjaro Queens ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii wametinga nusu fainali wakiwa wamefunga jumla ya mabao 20 kwenye mechi 3 za makundi huku wakiwa hawajaruhusu bao hata moja. 

Mchezo huo ulikuwa ni kama wakukamilisha ratiba tu kwani Kilimanjaro Queens walishafuzu kwenda nusu fainali wakati pia ndugu zao hao wa Zanzibar Queens wakiwa wameshatoka kabla hata ya mchezo huo.

Mabao ya Bara kwenye mchezo huo yamefungwa na Asha Rashid "Mwalala" na Donisia Daniel Minja waliofunga mawili kila mmoja.

Minja anakuwa amefikisha idadi ya mabao 6 ambayo yanamfanya kuwa kinara upande wa ufungaji kwenye michuano hii.

Mabao mengine yamefungwa na Diana Msewa, Phermena Daniel na Anastazia Katunzi.

Kilimanjaro Queens ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii wametinga nusu fainali wakiwa wamefunga jumla ya mabao 20 kwenye mechi 3 za makundi huku wakiwa hawajaruhusu bao hata moja. 

Bao Zanzibar wanarudi nyumbani wakiwa na furushi la jumla ya mabao 17 huku wao wakiwa hawajafunga hata bao moja.

Matokeo hayo yanaifanya Zanzibar kutolewa kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kupoteza mechi zote tatu kwa kufungwa jumla ya mabao 17, katika mechi tatu walizocheza huku wakishindwa kufunga hata bao moja.

Burundi Nao Wapenya

Kwenye mchezo wa mapema tumeshuhudia timu ya taifa ya Burundi wakiwaadhibu Sudan Kusini kwa kuwafunga jumla ya mabao 3-0.

Ushindi huo ni tiketi yao tosha ya kutinga nusu fainali ambapo sasa wamemaliza wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Kilimanjaro Queens kwenye kundi A.

Nani Kucheza Na Nani?

Timu za kundi A ambazo zimemaliza mechi zake itabidi zisubiri matoke ya kundi B ambapo kila mmoja atajua wakucheza naye.

Utaratibu uliopo ni kwamba kinara wa kundi A anacheza na mshindi wa pili kundi B. Na hivyo kinara wa kundi B anacheza na mshindi wa pili kundi A.

Kwasasa Uganda ni kinara wa kundi B akiwa anawaongoza Kenya kwa tofauti ya mabao lakini kwenye mchezo wa Alhamisi ambao unawakutanisha wao kwa wao ndiyo utatoa majibu ya msimamo wa kundi hilo.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed