AFCON 2021: Senegal, Nigeria Waanza Kwa Ushindi, Uganda Wapata Alama Ugenini

14th November 2019

DAKAR, Senegal- Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Sidy Sarr na Habibou Diallo yameiwezesha timu ya taifa ya Senegal kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Congo-Brazzaville

Nigeria
Nigeria
SUMMARY

Timu ya taifa ya Nigeria "The Super Eagles" wametoka nyuma na kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Benin mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Akwa ndani ya mji wa Uyo.

DAKAR, Senegal- Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Sidy Sarr na Habibou Diallo yameiwezesha timu ya taifa ya Senegal kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Congo-Brazzaville kwenye mchezo wa kwanza wa kundi I kuwania kufuzu Afcon 2012.

Ushindi huo umewafanya Segenal kuketi kwenye nafasi ya pili wakiwa nyuma ya Guinea-Bissau ambao wao kwenye mchezo wao wameshinda 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Eswatini.

Senegal au Simba Wateranga wanataka kusahau machungu yao ya Afcon iliyopita ambapo walifungwa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Algeria na badala yake wataka kuanza kwa kishindi kwenye kampeni hizi za kufuzu kwenye michuano ijayo itakayofanyika Cameroon.

Kocha Aliou Cisse alichagua kikosi chake kamili kwenye mchezo huo kikiwajumuisha wachezaji wake nyota kama vile Sadio Mane, Idrissa Gueye na Kalidou koulibaly, hata hivyo kuna wakati timu ilishindwa kucheza vizuri sababu ikiwa ni mazingira mabovu ya uwanja wa Thies.

Super Eagles Waepuka Aibu

Timu ya taifa ya Nigeria "The Super Eagles" wametoka nyuma na kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Benin mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Akwa ndani ya mji wa Uyo.

Stephane Sessegnon alianza kufunga bao kwa upande wa wagenini Benin lakini Victor Osimhen alisawazisha bao hilo ndani ya kipindi cha kwanza.

Bao la jitihada binafsi lililofungwa na winga anayecheza timu ya Bordeaux ya Ufaransa, Samuel Kalu lilisimama kama la ushindi kwenye mchezo huo ambao timu zote zilionesha uwezo wa hali ya juu.

Uganda Wapata Alama Ugenini

Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuondoka na alama moja kwenye ardhi ya ugenini baada ya kuwalazimisha wenyeji Burkina Faso kutoka sare ya 0-0 mchezo uliofanyika ndani ya jiji la Ougadouugou.

Kwenye mchezo huo Uganda walianza na wachezaji wao wote nyota kama vile nahodha Denis Onyango, Miya Farouk, Emmanuel Okwi na Joseph Ochaya.

Matokeo hayo yanawafanya Uganda kukalia nafasi ya pili nyuma ya Malawi ambao wao wameshinda kwa jumla ya 1-0 dhidi ya Sudan Kusini kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo la B.

Mechi ijayo itakuwa ni kati ya Uganda ambao watakuwa nyumbani kuwaalika vinara Malawi mchezo ambao utachezwa mapema wiki ijayo.

Kwenye ukanda wa Afrika Mashiriki, Uganda ni timu ambayo imefuzu kucheza Afcon kwa miaka misimu miwili mfululizo na kwasasa wanatafuta nafasi ya kushiriki mara tatu mfululizo tofauti na Kenya na Tanzania ambao wanasaka tiketi zao za mara ya pili tu.

Matokeo Mengine:

Namibia 2-1 Chad

Malawi 1-0 Sudani Kusin

Burkina Faso 0-0 Uganda

Sudan 4-0 Sao Tome

Angola 1-3 Gambia

Afrika Ya Kati 2-0 Burundi

Cameroon 0-0 Cape Verde

Guinea-Bissau 3-0 Eswatini

Senegal 2-0 Congo Brazzaville

Nigeria 2-1 Benin

Sierre Leone 1-1 Lesotho

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya