AFCON 2021: Hivi Ndivyo Nyota Wa Stars Walivyopambana Dhidi Ya Guinea

17th November 2019

DAR ES SALAAM,Tanzania- Taifa Stars jana ilianza vyema kampeni ya kufuzu Afcon ya 2021 huko Cameroon kufuatia ushindi wa 2-1 nyumbani

Taifa Stars
Taifa Stars
SUMMARY

Ni mshambuliaji ambaye taifa linajivunia kuwa naye alifanya kazi kubwa kwenye mchezo wa jana ikiwemo kufunga bao la kusawazisha huyu anatajwa kuwa ndio mchezaji bora katika mechi hiyo. Anapata 10.

Hapa chini Mtandao wa SportPesa News, unakuletea uwajibikaji wa kila mchezaji aliyecheza mechi ya jana.

Juma Kaseja

Huyu ni kipa mwenye uzoefu mkubwa na michuano hii ingawa kwa kipindi cha miaka sita alikaa pembeni lakini aliporudishwa bado ameonekana wamo.

Katika mchezo wa jana Kaseja, pamoja na kuruhusu bao moja lakini  hakupata kashkashi nyingi kivile.  Anapata 6.

Hassan Kessy

Kessy alicheza vizuri kiasi katika mchezo huo, uwezo wake wa kupandisha mashambulizi na kupiga krosi vilionekana na faida kubwa kwa Stars ingawa alitolewa kipindi cha pili kutokana na kuwa na kadi ya njano. Anapata 7.

Mohamed Hussein

Hakuna ubishi mlinzi huyu alitimiza vyema majukumu yake ndani ya uwanja, alizuia na kupanda mbele kupigackrosi ambayo moja ilizaa bao la kusawazisha liliofungwa na Simon Msuva. Anapata 9.

Kelvin Yondani

Huyu katika mchezo wa jana ilikuwa ngumu kujua anacheza nafasi gani kwani mpira ukiwa nyuma unamwona ukiwa mbele utamwona wakati mwingine alikuwa anapiga krosi kama beki wa kulia. Anapata 9.

Bakari Mwamnyento

Licha ya kwamba hana uzoefu wa kutosha na mechi za kimataifa lakini beki huyu alionyesha utulivu wa hali ya juu na kucheza mipira yote ya juu alikuwa ni kigingi imara kwa Kaseja. Anapata 9.

Erasto Nyoni

Kama ilivyokua kwa Yondani, Nyoni alicheza kwa kiwango bora sana jana na kuwadhibiti vyema washambuliaji wa Eguatorial Guinea. Anapata 9.

Mzamiru Yasini

Alicheza vizuri kwenye winga ya kulia na kusaidia eneo la kiungo alipiga pasi zilizofika kwa uhakika kwa wenzake na kupora mipira kwa wapinzani. Anapata 7.

Salum Abubakar 'Sure Boy'

Ndio mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo wa jana amefanya kazi kubwa ya kutawala eneo la kiungo hasa kipindi cha pili kwa kusambaza mipira mingi kwa washambuliaji wake.  Anapata 8.

Simon Msuva 

Ni mshambuliaji ambaye taifa linajivunia kuwa naye alifanya kazi kubwa kwenye mchezo wa jana ikiwemo kufunga bao la kusawazisha huyu anatajwa kuwa ndio mchezaji bora katika mechi hiyo. Anapata 10.

Mbwana Samatta

Pamoja na umwamba aliokuwa nao anapokuwa mbele ya lango la timu pinzani lakini jana Samatta hakuweza kuonyesha makali yake kivile licha ya kunyimwa penati ya wazi na mwamuzi. Anapata 7.

Farid Mussa

Jana ilikua mechi yake ya kwanza kuanza kwenye kikosi cha kwanza chini ya Etienne Ndayiragije kipindi cha kwanza hakuonyesha uboracmkubwa sana ukiacha pasi yake moja ambayo Msuva alishindwa kuitendea haki na kipindi cha pili alitolewa. Anapata 7.

Akiba

Ditram Nchimbi

Aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kessy alionyesha uhai mkubwa kwenye kushambulia na alipata nafasi mbili lakini hakuweza kuzitumia ipasavyo, hata hivyo alifanya kazi nzuri ya kutengeneza bao la pili lililofungwa na Sure Boy. Anapata 6.

Hassan Dilunga

Huyu ni kiungo wa Simba aliingia dakika za mwishoni kuchukua nafasi ya Farid Mussa, aliwezackufanya kazi yake  vizuri kwa dakika alizocheza. Anapata 5.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed